Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Dkt Mahile Njile pamoja na timu ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko Wilayani Ruangwa wamefanya mafunzo ya namna ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona. Mafunzo hayo yamefanywa Katika ukumbi ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, madiwani, timu ya menejimenti ya Halmashauri, watendaji wa Kata na viongozi wa dini.
Dkt Njile ameeleza kuwa Idara ya Afya imejipanga kukabiliana na ungonjwa huu na sasa kinachofanyika ni utoaji wa Elimu wa namna ya kujikinga kupata ugonjwa wa Corona, ametaja Kituo cha Afya Nkowe Kimetengwa maalumu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa endapo wakiwepo Wilayani Ruangwa.
”jamani tuacheni mizaha kila mmoja kwa sehemu yake achukue tahadhari za msingi ikiwemo kuacha kushikana mikono, kukumbatiana, kunawa mikono kwa sabuni kwa maji yanatotiririka hili si suala la kufanyia mizaha” amesema Dkt Njile
Aidha Dkt Njile ameeleza dalili za ugonjwa huo kuwa ni Joto kali kupita kiasi, Homa, mafua Makali, kukohoa, kuumwa kichwa, kubanwa mbavu, vidonda kooni na mwili kuchoka ni dalili za virusi vya Corona. Ameeleza kuwa mtu ukiona dalili hizo atoe taarifa kwa watoa tiba ili wafike kumuhudumia.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe Hashim Mgandilwa amewataka wananchi kuchukua hatua na tahadhari kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni.
Vile vile Amezitaka ofisi za umma na zisizo na umma kuweka maji ya kunawa na vitakasa mikono kwa ajili ya watumishi na zoezi hilo lifanyike katika nyumba za ibada yani makanisa na Misikiti.
“ kwa kipindi hiki watu mzingatie haya si ruhusa Kufanya Mikutano yote ya kisiasa ,kutofanyika, Harusi sherehe kama sio lazima sana ni vema isogezwe mbele, kwenda Magereza kutembelea ndugu na hata kufanya mikusanyiko isiyo na ulazima pia muache kupeana taarifa za taharuki kuhusu ugonjwa huu” amesema Mgandilwa
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa