Maafisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya yaRuangwa wamefanya kikao maalum leo Novemba 14, 2025, na Walambo, Ngariba pamoja na wamiliki waviwanja vya Jando na Unyago katika Ukumbi wa Mikutanowa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa. Lengo la kikaoni kujadili masuala ya uendeshaji wa shughuli za kijadikwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za serikali.
Akizungumza katika kikao hicho, Afisa Utamaduni waHalmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndg. Elias Ndamo, amesisitiza umuhimu wa wamiliki wa viwanja hivyokuhakikisha wanakata vibali halali kabla ya kuendeshashughuli zao. Aidha, ameeleza kuwa serikali inatarajiawamiliki kuwa na vitambulisho rasmi ambavyo vitasaidiakatika utambuzi na utoaji wa huduma pale kunapotokeachangamoto.
Ndamo amewataka wadau hao kuwa mabalozi wa kufuatasheria, kwa kuwaripoti watu wanaoendesha shughuli zakimila bila vibali au kukiuka taratibu zilizowekwa. Amesema hatua hiyo itasaidia kudhibiti vitendovisivyofuata miongozo ya serikali na kulinda usalama wajamii.
Aidha, Afisa Utamaduni huyo amefafanua kuwaHalmashauri itaanza kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wamara kwa mara ili kubaini wale wanaotekeleza shughulihizo bila kuwa na vibali au kutofuata utaratibu stahiki.
Katika maelekezo mengine, Ndamo amewasisitiza wadauhao kuzingatia kanuni za afya na maadili wakati wakuendesha shughuli za Jando na Unyago, ili kuzuiachangamoto za kiafya na kuepusha ukiukaji wa maadili yajamii.

Wakati wa mjadala, baadhi ya wajumbe walipata nafasi yakuuliza maswali, kutoa maoni na kupendekeza maboreshombalimbali. Wameipongeza pia Halmashauri kwa kuandaakikao hicho, wakieleza kuwa kimekuwa na manufaamakubwa katika kuongeza uelewa wa taratibu za serikalina kuimarisha ushirikiano katika masuala ya utamaduni.
Kikao hicho kilichojumuisha pia wataalam wengine kutokaKitengo cha Sanaa, Michezo na Utamaduni, kimehitimishwa kwa makubaliano ya kuendeleakushirikiana kwa ukaribu kati ya Halmashauri na wadauwa mila na desturi ili kuhakikisha shughuli za kimilazinafanyika kwa utaratibu, usalama na kuzingatia sheria.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa