Mkuu wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi
Elias Juma Nyerenga
UGAVI
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ina kitengo cha ugavi ambacho kumeundwa kwa mujibu wa sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kufugu na 37 ambapo sheria hiyo inaitaka taasisi ya serikali iwe na kiktengo cha ugavi (Procurement Management Unit –PMU).
Kitengo cha ugavi kinakiwa kiwe na mkuu wa kitengo mwenye elimu aliyosomea ujuzi huo na sifa, uzoefu katika kazi za manununzi na pia awe amesajiliwa na Bodi ya manunuzi (Procurement Professional Body).
Kwa mujibu wa sheria mkuu wa kitengo cha ugavi ataripoti moja kwa moja Afisa Masuhuli wa taasisi husika.
Afisa Masuhuli wa taasisi atahakikisha kwamba kitengo cha ugavi (PMU) kinatengewa fedha kwenye bajeti ili kiweze kutimiza majukumu yake.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UGAVI
Majukumu ya kitengo cha ugavi yameainishwa kwenye sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kipengele cha 38 kama yalivyo ainishwa hapa chini:-
Kitengo cha ugavi kinasimamia manunuzi yote toka idara na vitengo vilivyoko kwenye Halmashauri kitengo hiki kina wataalamu watatu (3) ambao wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.
Aidha kitengo cha ugavi mbali na kufanyakazi na idara na vitengo vya Halmashauri, pia kinafanya kazi kwa karibu sana kwa kushirikiana na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ambayo majukumu yake yameainishwa na sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kifungu cha 33 (1) (a) –( e).
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa