Ndg. Fundikira Masamalo
Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu
MIPANGO na UFUATILIAJI
Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatili ni mojawapo ya idara mama katika Halmashauri. Jukumu kubwa la idara hii ni kuratibu shughuli zote za maendeleo zinazotekelezwa na Halmashauri. Idara hii inawatumishi 4, aidha Idara hii haina kitengo bali ina seksheni kuu tatu ambazo ni mipango, takwimu na ufuatiliaji. Majukum na mafanikio ya utekelezaji wa majukum ya idara ya mipango ni kama ilivyoaininshwa kwenye jedwari hapa chini;
Jedwari; Majukum na Mafanikio ya Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji.
Na.
|
Idara/Kitengo
|
Sekisheni
|
Majukum
|
Mafanikio
|
|
Idara ya Mipango
|
Mipango
|
Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji (W) juu ya masuala ya uchumi na shughuli mbalimbali za maendeleo.
|
Mkurugenzi anashauriwa na idara zote juu ya masuala mbalimbali za kiuchumi. Hali hii imesaidia kuanzisha miradi mbalimbali mikubwa na ya kimkakati kama vile ujenzi wa ghala la wilaya, ujenzi wa uwanja wa mpira, uanzishwaji wa shamba la korosho la Halmashauri.
|
|
|
|
Kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
|
Halmashauri inatenga na kuchangia 60% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ngazi ya wilaya, kata na vijiji.
|
|
|
|
Kuandaa bajeti ya Halmashauri ya muda wakati.
|
Bajeti ya Halmashauri zinaandaliwa kila mwaka kwa kufuata muongozo na sheria ya bajeti.
|
|
|
|
Kuandaa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo.
|
Taarifa za shughuli mbalimbali za maendeleo zinaandaliwa na kuwasilishwa sehemu husika kwa wakati. Uandaaji na uwasilishwaji wa taarifa hizi kwa wakati unasaidia Halmashauri kupata hati safi.
|
|
|
Takwimu
|
Kukusanya takwimu mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo.
|
Takwimu zimekusanywa na kutumika kuandaa mpango mkakati wa Halmashauri kwa kuzingatia fursa za vikwazo katika Wilaya ya Ruangwa.
|
|
|
Ufuatiliaji
|
Kufanya usimamizi wa shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo.
|
Ufuatiliaji wa miradi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo unafanyika, taarifa za miradi hiyo zinaandaliwa na kuwasilishwa sehemu husika kwa wakati.
|
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa