Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa inapenda kutoa taarifa kuwa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwaimepata usajili rasmi na kuthibitishwa na Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) kama kituo cha kutoa mafunzo endelevu ya kitaaluma (CPD).
Aidha, cheti chenye namba ya usajili MCTCPDP260, kilichotolewa na MCT, ni uthibitisho wa ubora, uadilifu na uwezo wa hospitali katika kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kada mbalimbali za afya.
Hatua hii inalenga kuboresha huduma za afya, inaongeza ujuzi, maarifa na uwezo wa watoa huduma wa afya wa Wilaya ya Ruangwa na mkoa kwa ujumla.
Hivyo basi, Halmashauri inawapongeza wataalamu wote waliofanikisha hatua hii muhimu, na kwa hivyo inaendelea kujivunia maendeleo endelevu katika sekta ya afya.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa