Ndg. Charles Damian Tamba
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi
KITENGO CHA UCHAGUZI
Kitengo Uchaguzi ni moja kati ya Vitengo vilivyopewa hadhi ya Idara kamili. Kitengo hiki hufanya kazi za kuratibu shughuli zote zinazohusu Uchaguzi katika Jimbo. Kitengo cha uchaguzi kina majukumu mbalimbali kama ilivyoainishwa kwenye Jedwari hapa chini;
Jedwali: Majukumu na Mafanikio ya Kitengo cha Uchaguzi.
Na
|
Kitengo
|
Seksheni
|
Majukumu
|
Mafanikio
|
1
|
Uchaguzi
|
|
|
Jumla ya Chaguzi ndogo 3 za Madiwani zimeratibiwa kikamilifu na kuwezesha Kata za Mnacho, Nachingwea na Namichiga Kupata Madiwani wake ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka mshindi kwenye Kata zote tatu.
|
|
Kitengo kimejiwekea utaratibu wa kutunza nyaraka, vifaa na taarifa zote za Uchaguzi na kufanya uhakiki wa vifaa vyake kwa lengo la kuboresha kumbukumbu sahihi za mali za Tume.
|
|||
|
Kitengo kimekamilisha kuandaa vituo 187 vya kupigia Kura ambapo pia vimetumika kama vituo vya kujiandikisha wapiga kura. Aidha walengwa wanaotarajiwa kuandikishwa kwenye kipindi hicho ni wale ambao walikuwa na umri wa miaka 13-17 kwa mwaka 2015; jumla yao ni walengwa 19,356 ambapo wanaume ni 9931 na wanawake ni 9,125. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa maoteo ya sensa ya mwaka 2012.
|
|||
|
Jumla ya Rejesta 90 za Vijiji zimehuishwa.
|
|||
|
Nafasi wazi 163 za Viongozi wa Serikali za Vijiji 90 na Vitongoji 436 zimeratibiwa
|
|||
|
Kanuni zote zinazohusu Uchaguzi wa Serikali za Mtaa zimepitiwa upya na zingine zimefanyiwa maboresho ili kukidhi mahitaji ya wakati huu
|
|||
|
Wenyeviti wa Serikali za Vijiji vya Nahanga, Nangurugai, Chienjera, Dodoma, Makanjiro, Nangumbu ‘A’ na Kipindimbi wamerudi kwenye nafasi zao baada ya kufanya usuluhisho wa migogoro yao.
|
|||
|
Kitengo kimekuwa kikimshauri Mkurugenzi Mtendaji masuala yote ya Uchaguzi pamoja na kushirikisha Wakuu wa Idara zingine kwenye Vikao vya Wakuu Idara (CMT).
|
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa