SEKTA YA AFYA.
IDADI YA VITUO VINAVYOTOA HUDUMA ZA AFYA
: HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA
Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa imeweza kuongeza upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kutoka wastani wa 92% mwaka 2017/2018 hadi kufikia 94% Novemba 2018, ambapo lengo la kitaifa ni 80% kwa dawa muhimu.
Ongezeko hii la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Halmashauri yetu imechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Duka la dawa la MSD ambalo linatumika kutoa huduma za dawa na vifaa tiba katika zahanati, vituo vya afya na hospitali zote za mkoa wa Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru (mkoa wa Ruvuma) pamoja na upatikanaji wa Mshitiri wa Mkoa
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kupitia Idara ya Afya inajumla ya watumishi 271 sawa 30.4% ya watumishi 890 wanaohitajika ambapo upungufu ni sawa na 69.6%. Aidha Halmashauri inashukru serikali kuu kwa kuendelea kutoa kibali cha Ajira kwa watumishi kada za Afya na kuwapangia watumishi 62 kufanya kazi katika wilaya ya Ruangwa.
Halmashauri inaendelea kutekeleza mpango wa ujenzi wa vituo vya Afya kila Kata na Zahanati kwa kila kijiji kama ilivyoelekezwa katika sera ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Ujenzi wa Zahanati.
Jumla ya Zahanati 7 za vijiji vya Mihewe, Chikundi, Namkatila, Mkutingome, Namilema, Muhuru na Mbecha zinaendelea kujengwa na zinatarajiwa kukamilika na kufunguliwa kwa vipindi tofauti.
4.2.2 UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA VITUO VYA AFYA.
Kituo cha Afya Nkowe.
Ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha Afya Nkowe umekamilika kwa 100% kwa majengo ya vipaumbele ambayo ni nyumba ya Mganga, Jengo la Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia maiti, Maabara, Kichomea taka na Wodi ya Wazazi kwa kutumia fedha za uboreshaji wa miundombinu ya Vituo vya Afya kutoka Serikali Kuu shilingi 500,000,000.00.
Aidha hadi sasa kiasi cha shilingi 500,000,000 zimeshatumika kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya kituo.
Kituo cha Afya Mbekenyera.
Ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha Afya Mbekenyera umekamilika kwa 99.97% kwa majengo ya vipaumbele ambayo ni nyumba ya Mganga, Jengo la Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia maiti, Maabara, Kichomea taka na Wodi ya Wazazi kwa kutumia fedha za uboreshaji wa miundombinu ya Vituo vya Afya kutoka Serikali Kuu shilingi 500,000,000.00.
Aidha hadi sasa kiasi cha shilingi 499,853,870/= zimeshatumika kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya kituo.
Kituo cha Afya Mandawa.
Ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha Afya Mandawa umekamilika kwa 99% kwa majengo ya vipaumbele ambayo ni Jengo la Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia maiti, Maabara, Kichomea taka na Wodi ya Wazazi kwa kutumia fedha za uboreshaji wa miundombinu ya Vituo vya Afya kutoka Serikali Kuu shilingi 400,000,000.00.
Aidha hadi sasa kiasi cha shilingi 396,000,000 zimeshatumika kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya kituo.
5.0 UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imepokea kiasi cha shilingi 500,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya. Aidha taratibu za maandali ya uthamini wa eneo la ujenzi unaendelea.
6.0 WADAU MBALIMBAMBALI WA MAENDELEO KATIKA SEKTA YA AFYA
Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ina wadau mbalimbali wanaosaidia katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kama ifuatavyo;
S/N
|
JINA LA MDAU
|
KAZI WANAZOTEKELEZA
|
1
|
USAID BORESHA AFYA
|
Utekelezaji wa shughuli za UKIMWI, Malaria, TB na ustawi wa jamii
|
2
|
GIZ
|
Utekelezaji wa shughuli za CHF na Maboresho ya huduma za afya
|
3
|
KFW
|
Utekelezaji wa Mradi wa Tumaini la Mama
|
4
|
Mariestops
|
Utekeleza wa mradi wa uzazi wa mpango
|
5
|
PSI
|
Utekeleza wa mradi wa uzazi wa mpango
|
6
|
Sight saver
|
Utekelezaji wa mradi wa macho
|
7
|
ROPA
|
Utekelezaji wa shughuli za UKIMWI, Malaria, TB na ustawi wa jamii
|
8
|
MMAKIRU
|
Utekelezaji wa shughuli za Afya ya mama na mtoto
|
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa