Katika kutekeleza zoezi la vitambulisho vya wajasilimiamali kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa amewataka wajasilimiamali wadogo wadogo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kulipia na kupata vitambulisho vya wajasilimiamali .
Mkuu wa Wilaya ametoa tamko hilo katika kikao kazi kilichofanya mjini Ruangwa leo Desemba 22 katika ukumbi wa CCM kilichojumuisha watendaji kata , vijiji, makatibu tarafa, wakuu wa idara na kamati ya ulinzi na usalama.
Mheshimiwa Mgandilwa amesema vitambulisho hivyo vinapatikana kwa shilingi elf 20,000 ya kitanzania.
Amesema Mkuu wa Wilaya zoezi hilo litaanza rasmi Jumatatu 24/12/2018 na nizoezi la siku 9 mpaka tarehe 01/ 01/2019, mjasilimiamali anatakiwa kufanya malipo hayo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliyopo karibu na bank ya zamani ya NMB.
Aidha amesema zoezi hili ni lazima kila mjasilimiamali kuwa na hiko kitambulisho na asiyetii agizo hilo atakosa haki ya kufanya biashara ndani ya Ruangwa na sheria itafuata mkondo wake.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Andrea Chezue amewataka watendaji wa kata na vijiji kwenda kuwahamasisha na kuwapatia elimu ya faida ya kitambulisho hiko.
Pia amewataka wajasilimiamali wote waliondani ya Ruangwa mjini na vijijini kujitokeza kwa wingi kulipia na kuchukua vitambulisho hivyo kwa manufaa yao.
Pia amesema zoezi hili litawapima watendaji wa kata na vijiji kama wanafanya kazi yao ipasavyo kwa kubainisha wajasilimiamali wote wa maeneo yao.
Zoezi hili litawahusisha wajasilimiamali wote wadogo wadogo wa Ruangwa hata wamachinga, wanapaswa kulipia elf 20,000 kila baada ya mwaka mmoja na kwa kata zilizombali na Ruangwa mjini watafuata fomu katika ofisi za kata zao husika.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa