Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ndg, Rashidi Namkulala amewataka watendaji watakaokabidhiwa vitambulisho vya ujasiriamali kutimiza wajibu wao na si kukaa na vitambulisho ofisini.
Amesema hayo leo tarehe 27/05/2020 wakati akikabidhiwa vitambulisho hivyo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Kaimu Mkurugenzi amesema zoezi la ugawaji wa vitambulisho umeanza rasmi leo.
“zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivi litaratibiwa na ofisi ya Afisa biashara na pia vitapatikana katika ofisi za watendaji wa vijiji, gharama ya kila kitambulisho ni shilingi elf 20000 kama ilivyokuwa awali”
Aliendelea kuelezea vitambulisho vya awamu ya sasa vimeboreshwa na hata utaratibu wa ugawaji pia umeboreshwa mjasiliamali hatotoa fedha taslimu kwa mgawaji wa vitambulisho hivyo bali atalipia kwa mfumo wa bank au kupitia simu yake baada ya kupata control namba toka kwa muhusika anayemuhudumia
Aidha alielezea sifa za mjasiliamali anaepaswa kupata kitambulisho hiko ni yule ambaye mauzo ghafi yake hayazidi milioni 4 kwa mwaka.
“Kuna watu wanatumia vitambulisho hivi kufanya udanganyifu wananunua kwa kusema wamefirisika ili wakwepe kodi ya TRA safari hii tutawafuatilia kwa kina watu wenye kutaka kufanya udanganyifu kama huu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania” amesema Namkulala
akialika ushirikiano wa watendaji wa serikali watakaopewa kuuza vitambulisho hivyo amewataka kuhakikisha wanawaelimisha vyema wajasiriamali na kuwa waadilifu kwani watasaini fomu maalumu itakayoonesha idadi ya vitambulisho alivyopatiwa.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Gwamaka kalumbete alitoa rai kwa Wajasiliamali wa wilaya ya ruangwa kujitokeza kwa wingi kununua vitambulisho hivyo ambavyo Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli amewaandalia ili kutambulika na kuepuka usumbufu unaoweza jitokeza kwa kufanya shughuli zisizorasimishwa.
Alizitaka taasisi za fedha kutumia fursa hii kupata wateja wa mikopo midogo na kutoa elimu ya ujasiriamali na uwekezaji kwa kushirikiana na ofisi ya Afisa biashara kwani vitambulisho vya awamu hii vinaelezea shughuli ya mjasiriamali kwa upana zaidi.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa