Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania (TFRA) Kwa kazi ya kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi ya mbolea katika kuzalisha mazao mbalimbali, ameeleza kuwa kazi hiyo ni nzuri na yenye tija kwa Mkoa na Taifa. Pia aliwaomba TFRA waone umuhimu wa kutafuta na kuwaweka wakulima karibu zaidi na vifaa vya kupima udongo ili iwe rahisi kwao kufahamu mazao sahihi kwa udongo walio nao pamoja na mbolea sahihi.
Ameyasema hayo tarehe 12/04/2022 wakati wa maadhimisho ya siku ya mkulima iliyofanyika kijiji cha Chimbila B kilichopo kata ya Mnacho, maadhimisho yaliyobeba kauli mbiu ya "Tumia Mbolea kuongeza Kipato na Tija"
Mkuu wa Mkoa aliwataka TFRA kuendelea kuwashika mkono wakulima waliopata elimu ya mtumizi bora ya mbolea waweze kusaidiwa kupata mbolea kwa urahisi kwa misimu mitatu mfululizo na badae wakajitegemee na kua mabalozi wazuri kwa wengine.
Mheshimiwa Mkuu wa mkoa amewataka TFRA kusogeza huduma za upatikanaji mbolea kwa kuweka matawi mkoani Lindi ili mbolea zipatikane kwa urahisi kupitia halmashauri za mkoa wa Lindi kama ilivo mikoa mingine kuliko ilivo sasa wakulima huagiza kutoka wilaya za Masasi au Mtwara zinazopatikana mkoani Mtwara.
"Mnajua mkoa wa Lindi kuna maeneo kubwa sana la uzalishaji lakin bado tija ya uzalishaji ni ndogo hivyo tuwaelimishe wakulima wetu kutumia maeneo au mashamba tuliyonayo kwa kutumia mbolea ili tupate mazao ya kutosha"amesema Bi Zainabu
Vilevile Mkuu wa Mkoa amekemea kitendo cha kilimo cha kuhamahama badala yake amewataka wataalam wa kilimo washirikiane vizuri na TFRA kuwaelimisha wakulima kuhusu kuzalisha mazao vizuri kwa kutumia mbolea katika eneo hilo hilo.
"Wanahamahama kwasababa wanafanya kilimo cha kizamani cha bila kutumia mbolea mkiwasiadia wakulima wetu kuwapa elimu zaidi ya matumizi ya mbolea kilimo cha kuhamhama kitaisha Mkoa wa Lindi
Aliendelea kuwasisitiza maafisa ugani kutumia vifaa watakavyopewa katika kuwasidia wakulima kuanzia kupanda had kuvuna kwani hilo ni moja ya jukumu lao.
"mtapokea pikipiki 40 na zingine zitatolewa na bodi ya korosho hivyo zikatumike ipasavyo katika kutoa huduma bora za ugani, hizo pikipiki ni za kazi na si za kufanyia mambo binafsi zitumike kwa lengo husika" amesema Bi Zainab.
Mheshimiwa Zainab amewataka wakulima kuacha kuuza maua ya ufuta kipindi hiki na kusubiri ufuta uwe tayari ili wauze wakati wa msimu kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
" Haiwezekani mkulima atumie nguvu, akili, muda na fedha katika kuzalisha ufuta alafu auze maua sasa hivi kwa shilingi elfu moja alafu mnunuzi wa maua yeye akauze ufuta uliyotayari kwa shilingi 2,500/= jambo ambalo halikubaliki" amesema Bi Zainab.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania aliwataka wanakikundi walichopata elimu hiyo basi waendele kuitumia na kuwasaidia wengine ili kilimo cha mbolea kitumike kwa wingi na wakazi wa Ruangwa.
"Sisi tunajivunia sana kuwasaidia wakulima wa Ruangwa na hatutoishia njiani tutaendelea kuwasaidia mpaka tuhakikishe matumizi ya mbolea Ruangwa yamefanikiwa kwa asilimia zote" amesema Dkt Stephan Ngailo.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa