NA MWANDISHI WETU
Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Kilimo kutoka mikoa inayolima korosho, washirikiane kupata takwimu mpya za wakulima wa zao hilo.
Ametoa agizo hilo leo mchana jumapili, Desemba 31,2017) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji wa Mikorosho Bora na Mipya milioni 10 msimu wa 2017/ 2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.
“Maafisa Kilimo na Maafisa Ushirika mkisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, mshirikiane na kusimamia kwa umakini upatikanaji wa twakimu za wakulima na maeneo yanayolimwa, haiwezekani kila mwaka takwimu ziwe ni zilezile tu” alisema Waziri Mkuu
“Afisa kilimo wa Wilaya lazima ujue una wakulima wangapi, je hao wakulima wako, kila mmoja analima ekari ngapi? Na katika ekari hizo ana miche mingapi, na ana mahitaji ya pembejeo kiasi gani “alisema.
Pia nilikwisha waagiza maafisa ushirika na viongoi wa vyama vya msingi(AMCOS) mpaka chama kikuu cha ushirika, kuwa kila mmoja anapaswa atambue ana wanachama wangapi katika chama chake. Hili litawezekana pia kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au Mwenyekiti wa kijiji, kwasababu wao wanaidadi kamili za watu wanaowaongoza”alisema.
“Ninaimani tukifanya hili tutamaliza tatizo la takwimu na Serikali itakuwa nauwezo mkubwa wa kuwahudumia wakulima wake, tutaweza kuweka bajeti ya kutosha kuhudumia mahitaji yao”alisisitiza
Waziri Mkuu alipanda mche mpya wa korosho ili kuanzisha zoezi la upandaji miche hiyo na kisha kugawa miche kwa wakulima 10 kutoka Likunja, Kitandi, Kilimahewa na Nachingwea ambao waliwakilisha wenzao
Mapema kabla ya kuzungumza na wananchi Waziri Mkuu alikagua vitalu vya miche ya mikorosho vilivyopandwa na Halmashauri ya Ruangwa na kuelezwa kuwa miche hiyo ipo ya aina mbili ambapo aina ya kwanza ni ile iliyotokana na mbegu za pili iliyotokana na vikonyo
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa