• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

SERIKALI IPO IMARA NA INAENDELEA KUWAHUDUMIA WANANCHI-MAJALIWA

Posted on: November 18th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ipo imara na itaendelea kuhakikisha huduma mbalimbali za kijamii zinawafikia wananchi kwa ukaribu.

Amesema hayo leo Ijumaa (Novemba 18, 2022) alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, wilayani Ruangwa, Lindi

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuipa kipaumbele sekta ya afya kwa kuimarisha utoaji wa huduma na ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini lengo likiwa ni kusogeza huduma hizo karibu na wannachi

“Kituo cha afya cha Rais Samia kinakuwa na huduma zote muhimu zikiwemo za upasuaji, wodi ya wanawake na watoto, wodi za akinababa na akinamama, magonjwa mchanganyiko. Hii ndio dhamira yetu.”

Pia, Waziri Mkuu amesema ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya unaoendelea nchini unahusisha hospitali za rufaa za kanda, hospitali za rufaa za mikoa, hospitali za halmashauri, vituo vya afya na zahanati.

Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imesambaza wakandarasi wa umeme nchi nzima ikiwemo kwenye vijiji vya wilaya ya Ruangwa ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wote.

 

Katika hatua nyungine, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa wahakikishe wanabainisha wafugaji katika vijiji vyao ili kuwatambua pamoja na mifugo yao ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na migogoro ya wakulima na wafugaji.

 

Waziri Mkuu ametoa wito kwa wafugaji nchini kuweka utaratibu wa kufuga mifugo ambayo anaweza kuihudumia. “Hakuna mwenye haki zaidi ya mwenzake, ukiamua kufuga fuga mifugo ambayo unaweza kuihudumia, usilishe kwenye mashamba ya watu, kufanya hivyo mkono wa sheria utakufuata.”

 

Kadhalika, Waziri Mkuu amezitaka Serikali za vijiji kuhakikisha wanasimamia sheria ya kutolima ndani ya mita 60 kutoka kwenye mito na vyanzo vingine vya maji ili kuhufadhi vyanzo hivyo.

 

Akizungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mbwemkuru, Mheshimiwa Majaliwa amekipongeza kikundi cha vijana cha UKAJE UJENZI kwa kuamua kuanzisha umoja huo na kufanya kandarasi mbalimbali za Serikali.

 

Akizungumza kwa niaba ya Vijana wenzake, Mwenyekiti wa kikundi hicho amemshukuru Rais Samia kwa uamuzi wake wa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa fursa kwao ya kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.

 

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti, Wakazi wa Vijiji vya Nangurugai, Mbwemkuru na Narung’ombe wamemshukuru Rais Samia kwa fedha anazozitoa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya na elimu.

 

Mapema, Waziri Mkuu alitembelea familia zilizopoteza ndugu zao kutokana na tukio la wakulima na wafugaji kwenye kijiji cha Nambilanje. “Serikili itachukua hatua za kisheria kwa wote waliohusika na tukio hilo, tuendelee kuwaombea ndugu zetu, Serikali inatoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu zao.”

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA KATIBU MAHSUSI NA MTENDAJI WA KIJIJI June 26, 2022
  • Tangazo la uuzaji mahindi ya bei rahisi March 19, 2020
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI 23/ 08/2022 May 31, 2022
  • TANGAZO LA KUTAFUTA FUNDI UJENZI SHULE YA MPYA YA SEKONDARI KITANDI September 24, 2021
  • Ona zote

Habari mpya

  • SHULE YA MSINGI LIKUNJA KUJENGWA MADARASA 5 NA OFISI 2 ZA WALIMU.

    March 21, 2023
  • DC RUANGWA ASISITIZA UKUSANYAJI MAPATO

    March 01, 2023
  • NIMEFURAHISHWA NA MIRADI YA KIMAENDELEO - MAJALIWA

    February 22, 2023
  • SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI-MAJALIWA

    February 21, 2023
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa