Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani ambayo huazimishwa kila ifikapo June 5, kila mwaka Viongozi wa Wilaya ya Ruangwa kwa kushirikiana na wananchi wameanza maadhimisho hayo kwa kufanya mazoezi (jogging)na kufanya usafi eneo la wazi nyuma ya kwa Wanyumbani.
Mazoezi na usafi umefanyika leo June 1, 2024 ambapo mazoezi( jogging) yamefanyika kwa zaidi ya kilomita 5 na usafi umefanyika eneo la mraba zaidi ya hekari 1
Kwa mwaka 2024 kilele cha Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kimataifa yatafanyika katika jiji la Riyadh nchini Saudi Arabia, yakiongozwa na kaulimbiu " Urejeshwaji wa Ardhi iliyoharibiwa na ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame" Kaulimbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kuwa na matumizi endelevu ya Ardhi pamoja na kukabiliana na uharibifu wa ardhi zinazopelekea kuenea kwa jangwa na ukame.
Na kitaifa maadhimisho haya yatafanyika katika kituo cha mkutano Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kwa Mkoa wa Lindi kilele cha Maadhimisho kitafanyika katika Manispaa ya Lindi na mgeni rasmi atakayeshiriki shughuli za usafi anatarajiwa kuwa Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Lengo la Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali zake kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ametoa wito kwa wananchi kufanya mazoezi pasi shuruti ili kuimarisha Afya na kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka kwani mazingira yakiwa safi na Afya ikiwa imara watakuwa wamejiepusha dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa