Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mhe Rashidi Nakumbya amewataka wananchi wa Ruangwa kujitokeza kwa wingi tarehe 15/03/2020 katika mechi ya mpira wa miguu kati ya Namungo Fc na Yanga.
Amesema hayo leo tarehe 06/03/2020 wakati wa kikao cha baraza la Halmashauri lililofanyika katika ukumbi wa Rutesco Ruangwa mjini
Mhe Nakumbya amesema wanaruangwa wahamasike na kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya Namungo bila kujali kama ni shabiki wa yanga au simba
“Ukiwa ni mkazi wa Ruangwa itasikitisha sana mtu akianza kushangilia yanga siku hiyo jamani uzalendo kwanza Namungo kwanza tarehe 15 uwanja mzima uwe Namungo” Nakumbya
Aliendelea kusema Mhe Nakumbya hata mimi ni Yanga tena mwanachama mwenye kadi na si shabiki tu ila siku hiyo tarehe 15/03/2020 mimi ni Namungo na tutawafunga tu Yanga.
“Twendeni tukaujaze uwanja wetu twendeni tukashangilie Timu yetu tuachane hizi timu za wenzetu tupende vyetu Namungo ni timu ya wanaruangwa” amesema Nakumbya
Aidha alisema kutakuwa na usalama wa kutosha wa mali na watu hivyo amewaomba watu wajitokeze kwa wingi kutakuwa na usalama wa kutosha
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa