Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Elias Nkane, amewataka wakuu wa shule wanaopewa pesa kwa ajili ya kuongeza vyumba vya madarasa, chumba cha kukaa walimu na vyoo wazitumie pesa hizo kwa mahitaji yaliyokusudiwa.
Mh, Nkane Alisema pesa za lipa kulingana na matokeo (P4R) zinazopelekwa katika mashule ni nyingi hivyo zisiwatie tamaa wakuu wa shule na kuanza kuzitumia katika mipango isiyokusudiwa kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Mwenyekiti alisema hayo wakati wa ziara ya kamati ya huduma za jamii, zilipotembelea katika miradi katika kijiji cha Nachiungo, Mnacho, Chimbila B na Michenga, kamati ilitembelea shule ya msingi Nachiungo, shule ya sekondari Mnacho, mradi wa maji Michenga na kuangalia eneo la ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chimbila B.
Aidha Mwenyekiti aliutaka uongozi wa kijiji cha Chimbila A, kuhakikisha eneo walilotenga kwa ajili ya ujenzi wa zahanati alivamiwi na wanakijiji kwa ajili ya shughuli za kilimo na makazi,
``Jitahidi mpaka mwezi wa 8 mwaka huu zahanati iwe imesimama hata mkiomba nguvu kutoka Halmashauri itakuwa ni rahisi kusaidiwa, serikali ya kijiji mjitahidi katika kukusanya michango`` alisema.
Naye Diwani wa Mbwemkuru aliwasisitiza viongozi vya serikali ya kijiji cha Chimbila kukusanya michango ya ujenzi wa zahanati bila kuangalia wala kupendelea ili kuweza kifikia lengo walilojiwekea.
Katika kuonesha madiwani wako karibu na wananchi wao madiwani wawili waliweza kuchangia katika ujenzi huo bila kuangalia kuwa siyo kata yao, vilevile mganga mkuu wa Wilaya naye alichangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya dr Japhet Simeo aliwapongeza uongozi wa shule ya sekondari Mnacho kwa juhudi walizozionesha za kuanza ujenzi wa vyumba ya kukaa walimu ambavyo havikuwa katika mpango wa (P4R)kwani ni ubunifu mzuri walioufanya uongozi wa shule hiyo.
Pia aliwashauri uongozi wa kijiji cha Chambila B, kuwa na ushirikiano na jamii inayowazunguka kwasababu Wao ndiyo watu watakaoweza kusaidia kuendelea au kushia njiani kwa ujenzi wa zahanati hiyo
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa