Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ,Mhe, Rashidi Nakumbya amewata wakazi wa Wilaya ya Ruangwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa.
Amewataka wananchi kufanya kazi bega kwa bega na Mhe, Waziri katika kuleta maendeleo katika wilaya ya Ruangwa kwa Kushiriki shughuli za kimaendeleo alisema,maendeleo katika wilaya hii ni jukumu la kila mkazi wa eneo hili.
Alisema haya wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Mei 17 mpaka 18 katika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa.
Mhe, Nakumbya aliwataka waheshimiwa Madiwani wa Wilaya ya Ruangwa kuhakikisha wanatumia nafasi zao katika kuhamasisha wananchi wao katika kuchangia kufanya shughuli za kimaendeleo katika kata zao.
“Nisiwe mchoyo wa kushukuru kama watu wamefanya vizuri basi ni wajibu wangu kuwapa pongezi, nawapongeza wananchi wa kata ya Nachingwea na Ruangwa kwa kazi nzuri ya waliyoifanya ya kujitolea katika ujenzi wa shule ya mpya ya Sekondari Kassim Majaliwa” alisema Mhe, Nakumbya.
Aidha alimtaka Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue kuongea vizuri na wachimbaji wa visima waliopo katika wilaya kwa ajili ya kuchimba visima, waanze na shule ya sekondari mpya kwani ikianza bila maji itakuwa shida kwa wanafunzi na walimu.
“Shule yetu ni nzuri sana ila itaendelea kuwa nzuri pale maji yatakapopatikana, maji ni uhai hatuwezi kuanza kutumia shule hiyo bila kuwa na maji kwani itakuwa mateso kwa watoto wetu wakike pamoja na walimu ” alisema Mhe, Nakumbya.
Pia Mhe, Nakumbya aliwataka wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuhakikisha wanasafisha mashamba yao ya mikorosho ili mgao wa dawa ya kupulizia utakapofika kila Mkulima aweze kupata dawa hiyo na pia alisisitiza itazingatiwa zaidi kwa wale ambao wenye mashamba masafi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Mhe, Eliasi Nkane aliwaomba wakuu wa shule na Afisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha wanafuatilia sheria ya mtoto anayeaacha kwani watoto hawa wasipochukuliwa hatua inasababisha kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoacha shule.
“Zama za sasa imepunguza sana idadi ya watoto wa mitaani hivyo walimu na maafisa elimu ni wajibu wao kuwachukulia hatua watoto hawa wanaocha masomo ili tuzidi kutokomeza suala la watoto wa mtaani” alisema mhe Nkane.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa