Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe amekabidhi mbuzi 10 wa kufuga leo Juni 20, 2024 kwa Kikundi cha Ukombozi kilichopo kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa
Mbuzi hao wamepatikana baada ya Baraza la NACOFA kutembelea kikundi cha Ukombozi Mwezi 11, 2023 na kuahidi kuchangia shilingi Milioni 2 ili kukiimairisha kikundi hicho kupitia shughuli mbalimbali.
Kikundi hicho kimeanzishwa mwaka 2022 kikiwa na jumla ya wanakikundi 16 kikiwa na lengo la kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali kama vile kilimo na ufugaji pia kuimarisha afya kwa kuzingatia lishe bora.
Aidha, Mhe. Chikongwe ametoa wito kwa wanakikundi kutilia maanani mradi huo ili kupata matokeo chanya ya kimaendeleo katika kijiji na Kata kwa ujumla.
"Wenzetu wanatusaidia na wanataka matokeo chanya, hivyo basi wekeni mkazo kuhakikisha mbuzi hawa wanaongeza thamani ya kijiji chetu na musiwe na haraka ya kupata matokeo, hii itasababisha kuvuruga malengo"
Katika hatua nyingine, Mhe. Chikongwe amesisitiza mbuzi hao wakitunzwa vizuri watasaidia kupata samadi itakayosaidia katika shughuli za kilimo, pia kupata maziwa ambayo yatasaidia kuimarisha afya halikadhalika kusaidia wanakikundi kupata fedha mara baada ya mbuzi kuuzwa pindi watakapoongezeka.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Ukombozi Ndugu Siwazuli Ally Nkundi amelishukuru Baraza la NACOFA na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na kuahidi kuendeleza mradi huo ili iwe chachu ya maendeleo kwao na Wilaya kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa