Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa, Mwl. George Mbesigwe, ametoa fomu ya uteuzi kwa Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Zuwena Jabir Kitatichingi, katika ofisi yake leo, tarehe 22 Agosti 2025, tukio linaashiria rasmi kuanza kwa safari ya kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Kitatichingi amefika katika Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa zilizopo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, akiwa ameambatana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CUF pamoja na wanachama kadhaa wa chama hicho. Ujio huo ulivutia hisia kubwa kutoka kwa wafuasi waliokuwa wakimsindikiza, jambo lililoongeza hamasa ya kisiasa kuelekea uchaguzi ujao.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kitatichingi amesema hatua hiyo ni mwanzo wa safari yake ya kuwatumikia wananchi wa Ruangwa kwa kuzingatia changamoto zao na kusimamia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Aidha, kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi za ubunge unaendelea hadi Agosti 27, kabla ya uteuzi rasmi wa majina ya wagombea utakaofanyika kisheria.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa