Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Ruangwa Rashidi Namkulala amewataka mtandao usio wa mashirika ya kiserikali (MMAKIRU) kuwa waadilifu wa mradi wa kuwawezesha vijana kutekeleza Sera za umma ya Sera ya maendeleo ya vijana kwa njia ya majukwaa ya vijana.
Ametoa rai hiyo kwenye utambulisho wa mradi huo uliofanyika leo desemba 21 mjini Ruangwa katika ukumbi wa CCM uliohudhuliwa na watendaji wa vijiji na kata tatu, madiwani na watendaji wa halmashauri.
Namkulala amesema mradi huo umefadhiliwa na Foundation for Civil Society( FCS) ni wa shilingi milioni 49.5 ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kutekeleza Sera ya umma kupitia majukwaa ya vijana.
Afisa huyo aliwataka viongozi wa kata na Kijiji walioshiriki katika utambulisho huo wa mradi wakawe mabalozi wazuri katika kutoa elimu na lengo la mradi huo kwa vijana.
"Vijana wetu wanachangamoto nyingi mnatakiwa mjipange kukabiliana nazo ili mradi huu usije ukawa mradi hewa kama miradi mingine inayokwamishwa na vijana wenyewe " amesema Namkulala
Wakati huo huo Mwenyekiti wa bodi ya MMAKIRU aliiomba idara ya maendeleo ya jamii kuendelea mradi huo itakapofika mwisho wa wafadhiri kuwafadhili.
Alisema imekuwa ni desturi ya miradi kutelekezwa na serikali inapoisha hivyo anaiomba serikali kuuendeleza mradi huo pale utakapokuwa umefika mwisho wa kufadhiliwa.
Pia aliwaomba vijana kupokea mradi huo na kuutumia kwa kadri ya maelekezo watakayokuwa wanapokea na mabalozi wao, pia alichukua fursa hii kushukuru wafadhili wa mradi na kuwaomba waendele kuwasaidia pale wanapolekea miradi mingine.
Mradi huo ni wa shilingi milioni 49 na laki 5 umetolewa na wafadhiri na utawahusu vijana wenyewe rika la miaka 15 mpaka 35 na kwa kuanzia utaanza na kata 3 ambayo ni Nandagala, Nkowe na Mandarawe.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa