Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ameridhishwa na ufanyaji kazi wa watumishi sekta ya afya Mkoa wa Lindi katika kuzuia na kupambana na vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito.
Ameyabainisha hayo katika kikao cha Mkoa cha uchambuzi wa vifo vinavyotokana na uzazi kwa mama na mtoto kilichofanyika Juni 24, 2024 wilayani Ruangwa na kubainisha kuwa vifo vimepungua sana ukilinganisha na mwaka 2015/2016.
"Vifo vilikua 556, kama nchi tumefanikiwa kushusha hadi kufikia 104 huku watoto wachanga katika vifo 100 walifariki 67 tu kitaifa, ila kimkoa tumetoka vifo 47 vya wazazi mwaka 2021 hadi kufikia vifo 32 mwaka 2022 huku Kwa upande wa watoto wachanga vifo viliongezeka kutoka vifo 172 hadi 243 mwaka 2023 " Amesema Ngoma.
Kwa upande wake, Mganga mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Kheri Kagya amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa sana katika sekta ya afya nakupelekea kupunguza vifo vya mama na mtoto, huku akibainisha kuwa zaidi ya 97% ya wakina mama Mkoa wa Lindi wanajifungulia hospitali.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa