Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa amefungua mafunzo ya Mtaala mpya kwa shule za Sekondari Elimu ya Juu (Curricullum for Upper Secondary Education) leo Julai 8, 2024 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ruangwa.
Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo Jumatatu mpaka Jumatano na kuhusisha Walimu wa shule tano zenye wanafunzi wa kidato cha tano na sita na ni kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akilihutubia Bunge baada ya kuapishwa kwake kuwa Rais mwaka 2021 na kuiagiza Wizara ya Elimu kupitia upya Mitaala kama inakidhi vigezo na uhitaji wa wanafuzi.
Aidha, Ndugu Chonya amewataka Walimu kusikiliza kwa makini, kuwa watulivu ili wajifunze kikamilifu na wasisite kuuliza pale wasipoelewa, ili wanavyorudi kuwafundisha wanafunzi shuleni wafundishe kadri Mtaala unavyotaka.
Pia, amemuagiza Afisa Elimu Sekondari Ndugu Ernest Haule kuwapa posho Walimu wanaoshiriki mafunzo hayo ili kujikimu kwa siku hizi 3 za mafunzo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mafunzo hayo Ndugu Ali Juma kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa mapokezi mazuri na kutoa wito kwa walimu kuyazingatia yale watakayofundishwa ili kukuza sekta ya Elimu Tanzania.
Kwa niaba ya Walimu waliokuwa wanapata Mafunzo hayo Mwl. Hamis Kapera ameshukuru kwa mafunzo hayo mazuri yenye lengo la kuimarisha sekta ya Elimu Wilaya ya Ruangwa na Tanzania kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa