NA MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa amewataka viongozi waliochaguliwa wapya wa Amcos kufanya kazi kwa uadilifu katika kutekeleza majukumu yao alisema viongozi waliobahatikia kupata nafasi katika vyama vya Amcosi waitumie nafasi hiyo kwa kufanya vitu venye manufaa kwa wanaushirika na wanakulima wao.
Aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la kota ya nne lililofanyika Julai 28 mpaka 29 2017, katika ukumbi wa Rutesco Mjini Ruangwa.
Nakumbiya alisema kipindi kilichopita baadhi ya viongozi wa Amcos walitumia madaraka yao vibaya kwa kuhujumu mali za wanachama hali iliyopelekea wanachama kukosa amani na viongozi wao.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti aliwataka waendesha bodaboda kufuata sheria za barabarani kama zinavyoelekezwa na vyombo vya usalama.
“Vijana wetu wanajisahau sana huko barabarani na hasa vijijini ambako wanaona hakuna maaskari, wanabebana watu wanne pikipiki moja hili jambo ni hatari kwa usalama na maisha yao”alisema Mhe, Mkirikiti.
Pamoja na hayo mkuu wa wilaya alizungumzia rasilimali ya madini ambayo ina wawekezaji wengi na inakua kwa kasi sana wilayani Ruangwa akiitaka iangaliwe kwa undani ili kuepusha migogoro na upotezaji wa mapato ya serikali.” Watu wa madini tunatakiwa tuwaangalie kwa jicho la ndani zaidi” alisema Mh.Mkirikiti.
Aidha Mhe Diwani wa Kata ya Nandagala Chikongwe alitoa pongezi kwa Menejimenti ya Ruangwa nan a hasa Mkurungenzi Mtendaji kwa juhudi alizozifanya za kuiendesha Halmashauri.
“Wakati Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue anafikia katika Halmashuari hii aliikuta inamadeni mengi sana ila kwa uchapakazi wake aliweza kupunguza madeni hayo kwa kiasi kikubwa na kuifanya Halmashauri kuwa katika hali nzuri mpaka sasa”alisema Chikongwe.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa