Naibu katibu Mkuu Tamisemi Gerald Mweli anaeshughulika na masuala ya Elimu ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kukamilisha miundombinu katika shule ya Lucas Maria ili iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu.
Amesema hayo Leo 26/05/2020 wakati wa ziara yake ya kikazi Wilaya ya Ruangwa inayolenga kukagua miundombinu katika shule za mkoa wa lindi na maandalizi ya kupokea kidato cha sita ifikapo june 01/06/2020.
Naibu Mweli alitoa pongezi kwa ujenzi mzuri wa miundombinu katika shule ya Lucas Maria ambayo kwasasa shule hiyo ya Wasichana inatumika kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza tu.
“Shule nzuri sana hii mwaka huu naleta wanafunzi wa kidato cha tano, Mkurugenzi hakikisha unamaliza hayo mambo madogo madogo yaliyobakia, hii shule inasifa ya kuwa na kidato cha tano” amesema Mweli
“Siwezi kuacha watoto wetu wanakosa shule wakati tuna majengo mazuri sana hapa Lucas Maria vitu vilivyobaki ni vidogo sana muanze taratibu za kuomba usajili mtapokea kidato cha tano mwaka huu” amesema
Naibu katibu Mweli aliendelea kusisitiza suala la ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa miundombinu inayoendelea sasa katika Wilaya
“Zipo kazi ambazo wananchi wakihamasishwa wanaweza kuanza hata kabla fedha za ujenzi hazijaingizwa, hili likifanyika itakuwa rahisi kumaliza shughuli miradi inayoendelea” alisema
Vile vile aliagiza shule ya mbekenyera kutumia fedha za ukarabati wa miundombinu ya shule zinazopelekwa na Serikali kwa ajili ya kununua vifaa vikubwa vya kuhifadhia maji katika shule hiyo
“Maji ni uhai na maji ni muhimu hii shule inapaswa uwe na maji mpaka kwenye mabweni hizo fedha ambazo ziliingizwa kipindi hiki cha mapumziko zitumike kwa ajili ya kununua vifaa vya kutosha kuhifadhi maji hapo shule kwa kuzingatia sheria za matumizi ya fedha hizo” amesema
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa