Hewa tiba ni oksijeni safi inayozalishwa kwa kiwango cha kitaalamu kwa ajili ya matumizi ya kitabibu hospitalini. Hutumika kuwasaidia wagonjwa wenye changamoto za kupumua, akina mama wajawazito, watoto wachanga (hasa njiti), wagonjwa wa moyo, ajali na pia katika vyumba vya upasuaji. Ni sehemu muhimu ya huduma za dharura na tiba zinazookoa maisha.
Faida za hewa tiba ni pamoja na kuokoa maisha ya wagonjwa, kupunguza vifo vya watoto wachanga na akina mama, kuongeza ufanisi wa upasuaji na huduma za dharura, pamoja na kupunguza gharama na muda wa wagonjwa kusafirishwa kwenda hospitali za mbali. Upatikanaji wake katika hospitali za wilaya na kanda unaleta suluhisho la kudumu kwa changamoto ya uhaba wa huduma za kitabibu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa