Mkuu wa Mkoa Godfrey zambi, amewataka wananchi wa Ruangwa walio na umri kuanzia miaka 18 kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili kupatiwa vitambulisho vya taifa.
Ameyasema hayo siku za 23-24/01/2018 katika mikutano wa hadhara katika kata za Mandawa na Nanganga wakati wa Ziara yake ya kikazi aliyoifanya Wilaya ya Ruangwa.
Zambi amesema zoezi ili linaloendelea katika Wilaya ya Ruangwa ni wajibu na haki ya kila mwananchi kuwa na kitambulisho cha taifa hivyo mtu asijinyime haki hiyo na kusisitiza kuwa zoezi hili halihitaji gharama yoyote ya kifedha kwa mwanachi kujiandikisha .
Kwa kushiriki zoezi hili kutaliwezesha taifa kujua idadi kamili ya wananchi wake katika kile eneo na litasadia kuwezesha kutoa huduma kwa wananchi wake kwa kuzingatia takwimu za wakazi.
“Alitoa mfano kuwa Ruangwa ni wakulima wazuri wa kurosho ila kulikuwa na malalamiko ya pembejeo na mifuko ya kuhifadhia korosho hii imetokana na ukosefu wa idadi kamili ya watu usijinyime haki yako ya kupata vitu vinavyoletwa na serikali” Zambi amesema.
Naye Bi Sandra hamisi wa kijiji cha Mtakuja alisema walitangaziwa kuwa zoezi ni la bure lakini wanashangaa wanatozwa elfu tano ya picha ambayo wanashangaa sasa zoezi hili limekuwa si la bure tena.
“Ila zoezi hili limekuwa na muitikio mkubwa kwa wanakijiji wa eneo hilo, na wanaendelea kumiminika tunachoomba kupunguzwa kwa bei hii ya kupiga picha kwani ni kubwa watu wengi tunaitaji kitambulisho hicho cha taifa kwani wanatambua umuhimu wake” Bi Sandra alisema.
Katika kutolea ufafanuzi wa hela inayolalamikiwa na wananchi ,Afisa Usajili wa Wilaya Khalaf Mwalim, Amesema wakala wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanaendesha zoezi la uandikishaji na kutoa vitambulisho bure kwa wananchi pasipo kufanya malipo wananchi, na kusisitiza kuwa NIDA haimtozi mtu hela kwa ajili ya jambo lolote linalohusu utoaji wa kitambulisho.
“Ila ili mtu apate kitambulisho anatakiwa awe na kitambulisho na vyeti vya kuzaliwa ikitokea hana inabidi akapate utambulisho katika ofisi za Mtendaji wa Kata na utambulisho huo ndiyo unaokuwa na picha hivyo NIDA hatuhusiki katika hilo zoezi la upigaji picha ya kwenye barua ya utambulisho” Amesema Mwalim
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa