Katibu tawala mkoa wa lindi NGUSA SAMIKE amemuagiza mganga mkuu wa wilaya ya Ruangwa kuhakikisha mwishoni mwa mwezi septemba mwaka huu kufungua kituo cha afya Narungombe ambacho majengo kadhaa yamekamilika ujenzi wake kifunguliwe na kusisitiza apeleke wataalam katika kituo hicho ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo ya Jirani.
Hatua hiyo inakuja kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya septemba 24, 2022 ambapo katibu tawala huyo alikagua miradi ya ujenzi ya vituo vya afya na hospital ya wilaya ambapo katika wilaya ya Ruangwa ametembelea kituo cha Afya Narungombe na kukuta majengo mengi yamekamilika huku huduma ikiwa bado haijaanza kutolewa.
Kufuatia hali hiyo Samike Pamoja na kupongeza juhudi za uongozi wa Halmashauri ya Ruangwa kusimamia vizuri miradi hiyo ya ujenzi akatumia wasaa huo pia kuhimiza kufunguliwa kwa kituo hicho cha afya ili kutoa huduma kwa wananchi.
“Mmefanya kazi kubwa na nzuri sana nawapongeza sana mkurugenzi na timu yako, lakini mganga mkuu wa wilaya nikuagize mwishoni mwa mwezi huu hakikisha unafungua kituo ili kianze kutoa huduma kwa wananchi kwakua ndio lengo la serikali” alisema Katibu tawala Ngusa Samike.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Frank Chonya amekiri kupokea maelekezo ya kufunguliwa kwa kituo hicho mwishoni mwa mwezi septemba na kwamba tayari hatua za ufanyaji usafi katika majengo yatakayotumika zimeshafanyika hivyo kuahidi mapema Octoba mosi kituo hicho kitaanza kutoa huduma kwa wananchi.
Akieleza makadirio ya idadi ya wakazi wa kata ya Narungombe wanaotegemewa kunufaika na huduma ya kituo hicho Mganga mfawidhi wa zahanati ya Narungombe Gladyness Mwaindosia, amesema Zaidi ya watu 3,500 kutoka kata hiyo na maeneo ya Jirani watanufaika na huduma mbali mbali kituo hicho kitakapofunguliwa na kupunguza adha yavkusafiri umbali mrefu huku wananchi wa Kata hiyo wakiwamo Adila Musa akieleza tija ya kuokoa ghalama ya kusafiri umbali mrefu pindi kituo hicho kitakapoanza kutoa huduma.
“Mradi huu utasaidia kutupunguzia ghalama ya Kwenda ruangwa mjini ambako tulilazimika kukodi mapikipiki wakati mwingine tukikosa pesa tunatembea kwa miguu wagonjwa wanazidiwa njiana na wengine kufariki hasa wajawazito” alisema Adila mkazi wa Narungombe.
Mradi wa kituo cha afya Narungombe umeghalimu jumla ya shilingi milioni 500 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hiho cha afya ambapo miongoni mwa majengo yaliojengwa awamu ya kwanza ni Pamoja na jengo la wagonjwa wa nje, maabara,na kiteteketeza taka huku majengo mengine ya awamu ya pili yakiendelea kujengwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa