Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Ndugu Andrea Chezue ametoa shukurani kwa Kampuni ya Uranex inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya bunyu katika Wilaya ya Ruangwa kwa msaada wa bati waliotoa.
Mkurugenzi amepokea bati 266 kutoka kwa Uranex ambazo zitatumika katika kuwekeza madarasa matano na vyoo ambavyo vinajengwa katika shule ya sekondari mpya inayojengwa kwa nguvu za Wananchi, Halmshauri na misaada kutoka kwa wadau mbalimbali.
Aliyasema hayo wakati akipokea bati hizo kutoka kwa Meneja wa Uranes Mamboleo walipokuwa wanamkabidhi siku ya tarehe 11-02-2017 katika eneo la kiwanda cha kukamulia mafuta ya ufuta mjini Ruangwa.
Pia alisema Mkurugenzi "ujenzi wa vyumba vya madarasa umefikia katika hatua nzuri na unaenda kama ambavyo ilikuwa inategemewa na kesho wanaanza kupaua na kupiga mbao" aidha, aliwaomba Uranex waendelee na moyo huo huo wa kuweza kusaidia katika maeneo mengine wanatakapoombwa msaada.
''Tangu tumeanza ujenzi wa shule hii mpya Uranex tumekuwa nao bega kwa bega kwani walikuwa wanakwenda mara kwa mara kupitia katika eneo la ujenzi kuona hali ya kiujenzi inavyoendelea'' alisema.
Kampuni ya Uranex ilitoa msaada wa bati 266 kama ahadi waliyoitoa katika Ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alivyokuja mwezi wa Disemba mwaka 2016 ilyofanyika katika Wilaya ya Ruangwa
Naye Mkuu wa Wilaya Joseph Mkrikiti aliwaomba wadau wengine ambao hawajatoa ahadi walizoahidi basi waweze kutoa ili kuweza kufanikisha ujenzi huo kuisha mapema na Watoto waliokosa nafasi katika shule ya Ruanngwa Sekondari waanze masomo katika shule hiyo mpya.
Aidha, aliuomba Uongozi wa Halmshauri kutunza rasilimali wanazopewa kwa ajili ya ujenzi ili isiwavunje moyo wanaotoa misaada hiyo na kumuomba Mkurugenzi kuwa makini na matumizi ya vifaa hivyo vinavyotolewa na Watu.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya aliuomba Uongozi wa kampuni ya Uranex kutokuwachoka pale wanapokuiwa wanaitaji msaada kwani wao ni Watu wanaowategemea kufanya Ruangwa kuwa Ruangwa ya maendeleo.
Baada ya kupokea Msaada huo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na timu ya Wataalamu walioongozana nao waliweza kutembelea shule hiyo inayojengwa na uwanja wa mpira wa Nyasi bandia unaotegemea kujengwa Ruangwa mjini.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa