Kambi ya mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania( UMITASHUMTA) 2024 imefunguliwa rasmi leo Mei 19, 2024 katika ngazi ya Wilaya.
Ufunguzi wa kambi ya mashindano hayo umefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Dodoma Kata ya Nachingwea Wilaya ya Ruangwa ambao umehusisha Klasta tatu ambazo ni Namichiga, Ruangwa na Michenga kwa lengo la kutengeneza timu ya michezo ya Wilaya ambayo itajumuisha Wanafunzi 100 na Walimu 12 kwenda ngazi ya Mkoa hatimaye Taifa.
Kambi ya mashindano hayo itahusisha michezo mbalimbali kama vile Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Wavu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Miguu maalum, Sanaa za maonesho, Riadha maalum, Riadha za kawaida na mingine mingi.
Kwa upande wake msaidizi wa Waziri Mkuu Jimboni ambaye ni Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kambi wa mashindano hayo Ndugu Ramadhani Matola ametoa wito kwa wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo kujituma na kufanya juhudi kwani wana jukumu kubwa la kwenda kuiwakilisha Wilaya ya Ruangwa.
Aidha, Ndugu Matola amewaomba Walimu na viongozi wanaohusika na kambi ya mashindano hayo kuhakikisha nidhamu na kuwalinda watoto watakaochaguliwa kwenda ngazi ya Mkoa na hatimaye Taifa ili waweze kurudi nyumbani salama salimini.
" Malengo yetu ni kuwatengeneza vijana ambao wataenda kuleta ushindani Kimkoa na hata Taifa, hivyo tusifanye upendeleo kwenye kuwachagua wanafunzi watakaoenda kuiwakilisha Wilaya, tuchague wale ambao wanastahili" Amesema Matola.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa