Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa kata ya Mbekenyera Rashid Nakumbiya amewataka watendaji wa serikali za vijiji kufanya kazi kwa ushirikiano na kuacha tofauti za vyama,alisema jukumu la kiongozi kuitumikia jamii iliyompigia kura ni wajibu wa kila mmoja wao, aliwakata kujenga umoja kwa kuangalia masilahi ya wananchi waliowapiga kura kwa ajili yao.
Aliyasema hayo wakati akiongea na watendaji wa serikali za vijijini wakati wa ziara ya kutembelea Miradi ya kamati ya fedha Uongozi na Mipango,Iliyofanyika katika maeneo ya Chikundi, Namichiga, Namilema na Ruangwa mjini.Mwenyekiti alisema ushirikiano ni muhimu kwa pande vyama vyote vya kisiasa katika kuleta maendelea na wasifanye vyama vikawaga wao wote ni watanzania na sifa ya mwafrika ni umoja na ushikamano
Aidha aliuomba uongozi wa Halmashauri kuwafanyia utaratibu wa kupata tenki za maji katika shule ambazo zinauhaba wa maji ili waweze kuvuna maji ya kutumia wanafunzi kipindi cha ukame.Hata hivyo Mh.Nakumbiya alitoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri kwa kuweza kuwasaidia wanakijiji walioonesha nguvu zao na kuanzisha miradi ya maendeleo katika kata zao.Pia alitoa pongezi za kipekee kwa viongozi wa serikali za vijiji na wananchi kwa ujumla kwa kuweza kufanikisha zoezi la kuanzisha miradi kama zahanati na shule zao na kuwaomba wawe na moyo huo huo kwani maendeleo katika kijiji yanaanzwa kuletwa na wahusika wa eneo
Kamati ya Fedha na Uongozi na Mipango walitembelea mradi wa zahanati ya kijiji cha chikundi, ujenzi wa vyumba vya madarasa Namichiga sekondari, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Namileya na barabara za lami za mjini Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa