Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Godfrey Zambi aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kupata hati safi katika ukaguzi huo na kuwataka watendaji kuendelea kutimiza majukumu yao ya kila siku ili kupunguza hoja ambazo nyingi siyo nzito na uwezo wa kufanya hivyo sababu halmashauri hiyo ina viongozi na watendaji wachapakazi.
Amesema hayo leo 15/05/2020 katika Baraza maalum la kupitia hoja za ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2018/2019 lililoanyika katika ukumbi wa Narungombe Pub Ruangwa mjini na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa, wageni kutoka ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Pia amewataka waheshimiwa Madiwani kuendelea kushirikiana katika utendaji kazi ambao umeleta matunda na kupata hati iliyosafi
“Hakuna kizuri kama ushirikiano katika kutekeleza majukumu mkiendelea hivi mtafika mbali mkifanya kazi kwa pamoja mtaifikisha mbali zaidi Halmashauri kwa upande wa maendeleo ya Wilaya”amesema Zambi.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa kuwashugulikia wafanyabiashara wanaoficha sukari na wanaouza bei ya juu na atakaebainika basi sukari yake itaifishwe na iuzwe bei elekezi ya serikali ya shilingi elf 2800.
“Tumebaini kuwa hakuna uhaba wa sukari bali ni wafanyabiashara wanaficha sukari kwa lengo la kuuza sukari kwa lengo la kuiuza kwa bei kubwa
Mheshimiwa Zambi alisema wakazi wa Ruangwa wasiwe na hofu kwani sukari ya kutosha imeshushwa jana alhamisi bandarini hivyo suala linaloendelea sasa la kupanda bei ya sukari kiholela limeisha.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa Bi Rehema Madenge amewataka wananchi Kuendelea kujikinga na virusi vya ugonjwa wa corona na kuchukua tahadhari kama maelekezo yanavyotolewa na wataalamu wa afya
Pia ameitaka menejiment ya wilaya kuhakikisha inafuatilia suala la ukusanyaji mapato Na kuhakikisha watu wanaokusanya mapato wanafikiwa mara kwa mara kwa ukaguzi.
“Msisubiri watu wenye POS walete makusanyo huku ofisi kuu wafuatilieni huko huko msibweteke kabisa suala la kukusanya mapato ni la watumishi wote na si watu wachache shirikianeni” amesema bi Madenge
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa