Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa amewataka wananchi wote wa Wilaya ya Ruangwa kujitoa hali na Mali katika kuchangia shughuli za maendeleo zinazoendelea katika maeneo yao.
Ameyasema hayo alipokuwa kwenye muendelezo wa ziara zake katika kata ya Nandagala siku ya tarehe 04/ 12/2018 alipokuwa akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
Mhe. Mgandilwa amewataka wananchi kuanza kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yao ambazo aziitaji fedha mfano barabara ambayo inahitaji nguvu kazi kwa kukata visiki na kutoa manyasi.
" Tusisubiri kuletewa maendeleo tuanze wenyewe kuyaleta najua maeneo mengi mnaupungufu wa vyumba vya madarasa anzeni kufyatua matofali na ujenzi wa awali, Serikali itatia nguvu kazi kama sehemu nyingine"
"Mtakapopanga siku yakufanya hizo kazi nipeni taarifa nitakuja kufanya kazi na nyie na mie ni kiongozi nisiyependa kukaa ofisini nitakuja na watu wangu kwani sisi viongozi ndiyo tunapaswa kuwa mfano" alisema
Kuhusiana na Ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mnacho Mhe. Mgandilwa amewataka wakazi wa kata ya Nandagala kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Mnacho
Kwani kukamilika kwa Ujenzi huo kutapunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu
"Ujenzi wa mabweni katika shule ya Mnacho ni jukumu la kila mkazi wa kata ya Nandagala na Mnacho najua vipo vitu mmekubalina kufanya vya kimaendeleo vya kata zenu na ni vya umuhimu ila ujenzi wa mabweni ni muhimu zaidi" amesema Mgandilwa
Vilevile Mkuu wa Wilaya ametoa onyo kwa wanawake wote ambao wanacheza michezo ya kukaa uchi katika sherehe mbalimbali zinazofanyika katika Wilaya ya Ruangwa
Nipeni taarifa ya mtu yoyote anaefanya hiyo michezo ya kukaa na kucheza michezo isiyokuwa na maadili nitakushughulikia nikikubaini.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa