Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hashim Mgandilwa amewataka wanaume wa Ruangwa waliowaachisha masomo watoto wa kike na kuwaoa kufika kituo cha polisi kesho asubuhi.
Ametoa agizo wakati wa ziara yake Leo 08/10/2018 ya kujitambulisha aliyoifanya katika kata ya Mbwemkuru katika vijiji vinne ambavyo ni Chiundu, chikwale, nangurugai na machanyanja.
Mheshimiwa Mgandwila amewataka wanaume wanaoishi na wanafunzi waliowakatisha masomo kuanzia mwaka 2015 mpaka 2018 wajisalimishe wenyewe kesho kituo cha polisi mjini Ruangwa.
"Wanawake wa kuoa wako wengi katika maeneo yenu kwanini mnawaharibia wanafunzi masomo amuwaoni huruma wazazi wa hao watoto mnaowaharibia maisha" amesema Mgandilwa
" Niachieni watoto wangu acheni wasome nawao waje kuwa na nafasi kama za juu za uongozi nasema nitakula sahani moja na hawa watu wanaoniharibia wanafunzi" amesema Mgandilwa.
Pia Mkuu wa Wilaya alisema na kuna wazaz waliopokea rushwa kumaliza kesi za watoto wao waliopata ujauzito nataka niwaambie nikimalizana na hawa walioweka mimba nakuja kuanza na nyie.
" na nyie mliotoa Rushwa na kuharibu kesi nawapa salamu zangu kesi hizo zitaanza upya sitofumbia macho suala hili hamuwezi ishinda serikali na amuwezi kuwa juu ya serikali nyie amesema Mgandilwa.
Mheshimiwa aliwakumbusha wananchi kuwa kitendo cha kumpa mimba mwanafunzi ni kifungo cha miaka 30 jela aliwataka kuacha kuwaharibia masomo wanafunzi.
Naye kaimu Afisa elimu Sekondari mwalimu Nassu Anna aliwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao wa kike na kuwapatia elimu ya kujitambua ili kupunguza mimba shuleni.
Alisema mwalimu Nassu wazazi watambue wajibu wao kwa kuongea na mabint zao kama wanavyofanya walimu wakiwa shuleni kuongea na wanafunzi kwa kuwapa elimu na kuwaonesha umuhimu wa elimu.
"Anachokifanya Mkuu wa Wilaya ni jambo zuri sana na jema na litasaidia kupunguza mimba mashuleni aendele na msimamo huohuo kwani inawezekana kuwa na Ruangwa isiyo na mimba shuleni" amesema mama nassu.
Mwalimu Nassu alisema kwa mwaka wa masomo 2017 mpaka 2018 wanafunzi waliopata ujauzito ni 18 hali hii si nzuri aliwaomba walimu na wazazi washirikiane katika kupunguza na kuondoa tatizo hilo
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa