Benki ya NMB tawi la Ruangwa imefanya kikao na timu ya Menejimenti ya Wilaya ya Ruangwa (CMT), leo Juni 28, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Lengo kuu la kikao hicho ni kudumisha uhusiano mzuri kati ya Benki ya NMB na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, pamoja na kutoa elimu kwa watumishi kuhusu umuhimu wa kuweka akiba na upatikanaji wa mikopo.
Aidha, Katika kikao hicho viongozi wa NMB wametoa elimu kuhusu faida za kuweka akiba kwa watumishi wa umma na jinsi wanavyoweza kunufaika na mikopo inayotolewa na benki hiyo. Kikao hicho kimejadili pia njia mbalimbali ambazo benki inaweza kushirikiana na Halmashauri katika miradi ya maendeleo na kuboresha huduma za kifedha kwa wananchi.
Sambamba na hayo, wamejadili mbinu za kuboresha ushirikiano katika kutoa huduma bora kwa wateja na kuhakikisha kuwa watumishi wanapata elimu stahiki kuhusu masuala ya kifedha, ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya mikopo na mbinu za kuwekeza ili kujenga maisha bora ya baadae.
Ikumbukwe Benki ya NMB imekuwa na kawaida ya kufanya vikao na halmashauri vyenye lengo la kujenga mahusiano kati ya NMB na Halmashauri, na kuweka msingi mzuri wa ushirikiano endelevu ambao utawasaidia watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na wananchi kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa