Timu ya ASHALONGO FC ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imeibuka kidedea kwa penalti 6–5 dhidi ya Timu ya Afya FC baada ya sare ya 2–2, katika Bonanza la Siku ya Afya lililofanyika Majaliwa Stadium leo 27 Julai 2025.
Bonanza hilo la maadhimisho ya siku ya afya limeandaliwa na Idara ya Afya Wilaya ya Ruangwa kwa lengo la kuimarisha afya za watumishi, kujenga mshikamano kazini, na kukuza mahusiano chanya baina ya idara mbalimbali za Halmashauri kupitia michezo.
Mbali na burudani ya soka, tukio hilo limevutia umati wa watu na kuambatana na shamrashamra, ushirikiano wa kijamii na ujumbe wa kuhimiza mtindo bora wa maisha. ASHALONGO FC limezawadiwa mbuzi kama heshima ya ushindi huku mashabiki wakilipuka kwa shangwe na vifijo.
Mbali na mechi hiyo ya kusisimua, bonanza limeambatana na michezo mbalimbali, shamrashamra, burudani, na ujumbe wa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa afya na ushirikiano kazini. Tukio hilo limeacha alama chanya kwa washiriki na mashabiki waliouhudhuria kwa wingi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa