Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ruangwa Ndugu Rashidi Namkulala ametamatisha mafunzo ya kuwajengea wanawake uwezo kiuchumi na uongozi leo Juni 30, 2024 katika Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa.
Mafunzo haya ni Mradi uliofadhiliwa na Shirika la @unwomen wenye lengo la kuongeza uelewa na ushawishi kwa viongozi wa dini, viongozi wa mila na wananchi kwa ujumla katika kumkomboa mwanamke kiuchumi na kumuwezesha kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Aidha, Ndugu Namkulala ameongeza kwa kusema kuwa uwazi, uaminifu, imani na uvumilivu ni chachu ya maendeleo katika familia.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa