• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

MICHE BORA 175,701 YA KOROSHO KUWANUFAISHA WAKULIMA RUANGWA

Posted on: February 19th, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa miche bora ipatayo 175,701 ya mikorosho kwa wakulima waliosajiliwa na Ofisi ya Kilimo, kata na vijiji Wilayani humo, ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la korosho msimu wa 2025/2026.

Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 19 Februari, 2026 katika vitalu vya uzalishaji miche ya mikorosho vilivyopo Kijiji cha Kilimahewa kata ya Nachingwea. Akizungumza katika hafla hiyo, DC Ngoma amesema ugawaji huo ni hatua ya kimkakati katika kuimarisha uchumi wa wananchi na kuongeza tija ya zao hilo ambalo ndilo tegemeo kuu la Wilaya ya Ruangwa.

“Korosho ni uti wa mgongo wa uchumi wa Wilaya yetu hivyo miche hii ikitunzwa vizuri itaongeza uzalishaji, kipato cha mkulima mmoja mmoja na mapato ya Halmashauri. Ni wajibu wetu kuhakikisha kila mche unapandwa na kuendelezwa kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo,” amesema Mhe. Ngoma.

Katika taarifa yake Mkuu wa Idara Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg. Thadei M. Luoga amebainisha kuwa lengo la Halmashauri kwa msimu huu lilikuwa kuzalisha miche 200,000, ambapo hadi sasa miche 175,701 imezalishwa kupitia vikundi saba(7) vya uzalishaji vilivyoingia mkataba na Bodi ya korosho ndani ya Wilaya na kuanza kugawiwa bure kwa wakulima waliosajiliwa rasmi.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Ruangwa ina wakulima wa korosho 23,588 wenye miti 5,543,028 katika eneo la hekta 73,907. Zao la korosho linachangia zaidi ya asilimia 85 ya mapato ya wananchi. Katika mwaka wa fedha 2025/2026, zao hilo limeingizia Halmashauri zaidi ya shilingi bilioni 1.6, huku wakulima wakilipwa zaidi ya shilingi bilioni 80.1 kutokana na mauzo ya korosho ghafi.

Aidha, tathmini ya misimu minne kuanzia 2022/2023 hadi 2025/2026 inaonesha jumla ya miche 454,812 imezalishwa na kugawiwa kwa wakulima. Jumla ya ekari 5,856 zinatarajiwa kupandwa katika awamu hii, huku Ofisi ya Kilimo ikiendelea na usimamizi na ufuatiliaji wa upandaji na ukuaji wa miche hiyo ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya yaliyokusudiwa.

Matangazo

  • NAFASI ZA KUJITOLEA HALMSHAURI YA WILAYA YA RUANGWA February 13, 2026
  • FOMU YA USAJILI WA WAANDAAJI WA MAUDHUI MTANDAONI February 02, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 25, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MICHE BORA 175,701 YA KOROSHO KUWANUFAISHA WAKULIMA RUANGWA

    February 19, 2026
  • IDARA YA MAENDELEO YA JAMII YAGAWA KOMPUTA MPAKATO KWA MAAFISA MAENDELEO RUANGWA

    February 19, 2026
  • RUANGWA YATOA ZAIDI YA TSH MILIONI 420 YA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI (10) KWA MAKUNDI MAALUM

    February 19, 2026
  • NGUVU YA HAZINA YA MADINI INAYOBADILI HATIMA YA WANARUANGWA

    February 11, 2026
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)
  • Watumishi Portal

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa