• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

RUANGWA YATOA ZAIDI YA TSH MILIONI 420 YA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI (10) KWA MAKUNDI MAALUM

Posted on: February 19th, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, ameshiriki hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, ikiwa ni sehemu ya mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia asilimia kumi (10%) ya mapato ya Halmashauri.

Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 18 Februari, 2026 katika bwalo la Shule ya Sekondari Ruangwa Girls na kuhudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Katibu Tawala wa Wilaya, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya, Katibu wa Mbunge, Wakuu wa Idara na Vitengo, pamoja maafisa wa TAKUKURU na wawakilishi wa taasisi za kifedha (NMB Bank)

Akiwasilisha taarifa ya utoaji wa mikopo hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Mwl. George Mbesigwe, amesema kuwa katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, Halmashauri imetoa jumla ya shilingi 420,877,000 kwa vikundi 71 vya makundi maalum. Kati ya fedha hizo, vikundi 37 vya wanawake vyenye wanufaika 198 vimekopeshwa shilingi 164,636,000. Vikundi 24 vya vijana vyenye wanufaika 130 wanaume 113 na wanawake 17 vimekopeshwa shilingi 232,541,000. Aidha, vikundi 10 vya watu wenye ulemavu vyenye wanufaika 15, wanawake 3 na wanaume 12, vimekopeshwa shilingi 23,700,000.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya Mhe. Ngoma amesema, "Mikopo hii ya asilimia kumi ni fursa muhimu ya kuwawezesha wananchi kiuchumi. Ni wajibu wa kila kikundi kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, kuendesha miradi yenye tija na kurejesha kwa wakati ili na wengine wapate kunufaika. Nidhamu ya fedha ndiyo itakayofanya mpango huu ulete matokeo halisi katika maendeleo ya Ruangwa".

Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo wametoa shukrani kwa Serikali kwa kuwawezesha mitaji ya kuanzisha na kukuza miradi ya kiuchumi, wakiahidi kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuzirejesha kwa wakati.

Matangazo

  • NAFASI ZA KUJITOLEA HALMSHAURI YA WILAYA YA RUANGWA February 13, 2026
  • FOMU YA USAJILI WA WAANDAAJI WA MAUDHUI MTANDAONI February 02, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 25, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • IDARA YA MAENDELEO YA JAMII YAGAWA KOMPUTA MPAKATO KWA MAAFISA MAENDELEO RUANGWA

    February 19, 2026
  • RUANGWA YATOA ZAIDI YA TSH MILIONI 420 YA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI (10) KWA MAKUNDI MAALUM

    February 19, 2026
  • NGUVU YA HAZINA YA MADINI INAYOBADILI HATIMA YA WANARUANGWA

    February 11, 2026
  • ASHALONGO FC VS KIBWANA FARM FC, HAKUNA MBABE

    February 08, 2026
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)
  • Watumishi Portal

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa