Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Limepitisha makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kiasi cha shilingi bilioni 30,886,546,499.57 huku mapato ya ndani yakiwa ni asilimia 16% tu, kutokana na hali hiyo watendaji katika halmashauri hiyo wamehimizwa weledi na uadilifu katika ukusanyaji wa mapato ili kuyafikia malengo waliyojiwekea.
Wakizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo mwenyekiti wa baraza la halmashauri wilaya ya Ruangwa ANDREW CHIKONGWE amesema bajeti iliopangwa inahitaji kutekelezwa kwa vitendo katika ukusanyaji wa mapato na kuagiza kuwachukulia hatua wale wote wanaokwamisha ukusanyani huo, huku mkuu wa wilaya ya Ruangwa HASSAN NGOMA akiwataka madiwani na watumishi kushikama kwa pamoja ili kuyafikia malengo waliojiwekea.
"Kwa bajeti hii sisi tunachangia asilimia chache tu kutokana na makusanyo yetu maana yake serikali ikituacha tujitegemee tutakwama, kwahiyo tuna kila sababu ya kuongeza nguvu katika kukusanya mapato ili tujitegemee." Alisema Chikongwe ambae ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa.
Aidha akieleza mikakati waliojiwekea katika kuhakikisha bajeti hiyo inafikiwa kikamilifu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Ruangwa Ndgu. Frank Fabian Chonya, amesema wameshaanza kuchukua hatua kwa wanaokwamisha ukusanyaji wa mapato wilayani humo, huku Ndugu, Juma chikunda ambae ni katibu wa chama cha wananchi CUF aliyehudhuria baraza hilo kama mjumbe mwalikwa akipongeza kwa mapendekezo ya bajeti hiyo kwa kueleza kuwa imegusa kila sekta ya maendeleo wilayani humo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa