Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vyumba vya madarasa mawili vilivyokamilika vikiwa na madawati kutoka kwa bank ya CRDB.
Amepokea madarasa hayo leo Desemba 31/ 2018 katika shule ya Sekondari Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea Ruangwa mjini.
Amesema Waziri Mkuu jambo walilolifanya bank ya CRDB ni kubwa sana kwani kwa kipindi hiki Wilaya inakumbwa na tatizo la watoto waliofaulu ila wamekosa shule za kujiunga na kidato cha kwanza.
"Wanafunzi 230 hawajapangiwa shule kwa sababu ya uhaba vyumba vya madarasa kutokana na msaada huu, uhaba katika shule hii utakuwa umeisha" amesema
Wilaya ina shule 16 za sekondari zinazohudumia watoto wote wa Ruangwa ila shule hizi hadhikizi mahitaji na kutokana na ongezeko la ujenzi wa shule mpya katika Wilaya zikikamilika idadi ya shule zitakuwa 26 itapelekea kukidhi mahitaji ya watoto wa Ruangwa.
" Ruangwa ya sasa si ya zamani wazazi wamekuwa na mwamko wa elimu ndio maana ongezeko la ujenzi wa shule na wananchi kujitolea kushiriki ujenzi umekuwa mkubwa niwatake muendele na hali hiyo hiyo" amesema.
Pia amezitaka taasisi nyingine za kifedha waige mfano wa bank ya CRDB kwani imekuwa bega kwa bega katika kuchangia shughuli za kimaendeleo Wilayani Ruangwa.
Aidha, ametoa wito kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kassim Majaliwa kutumia vizuri madarasa hayo na kutunza mali zilizopo shuleni hapo.
Amesema " nategemea hii shule baadae ije kuwa na kidato cha tano na Sita hivyo yatunzeni madarasa yenu na mali zilizopo hapo shuleni ili itakapofika kipindi cha shule kupata sifa ya kuwa na kidato cha 5 na 6 kusiwe na marekebisho ya madarasa".
Wakati huo huo Waziri Mkuu amekabidhi computer 20 kwa shule za sekondari 5 ambazo ni Kassim Majaliwa, Likunja, Mnacho, Hawa mchopa na Ruangwa.
Amekabidhi computer hizo hizo kwa uchache kutokana na shule hizo kutokuwa na nyumba maalumu vya kuhifadhia.
" Bado zipo computer nyingi walimu wakuu nendeni mkaandae vyumba maalumu vya kuhifadhi computer ili mkabidhiwe zilizobaki.
Waziri Mkuu yupo Wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku 4 kuanzia tarehe 30 Desemba 2018 mpaka 02 januari 2019.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa