Katika kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Ndg, Andrea Chezue ameamua kuwapima watendaji wa kata na Kijiji kwa kuwashindanisha kutokana na utendaji kazi wao wa kila siku.
Amesema hayo Desemba 22 wakati wa kikao cha watendaji kilichofanyika mjini Ruangwa katika ukumbi wa CCM.
Mkurugenzi huyo amesema zoezi hilo litaanza rasmi January 2019 na atatoa vigezo vya kuwapima watendaji hao na mshindi atapokea zawad itayokuwa imeandaliwa.
Amesema Ndg,Chezue kuwa kwa upande wa elimu shule za msingi walifanikiwa mwaka huu kwa sababu ya kuwashindanisha walimu hali iliyopelekea Ruangwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa.
"Sasa nakuja kwenu watendaji na sitoishia kwa watendaji kata na vijiji tu nitafika mpaka kwenye kada nyingine ila awamu hii naanza kata na vijiji na nitawapima kwa utendaji kazi wenu" amesema Chezue.
Pia amesema kila mtendaji aanze kujitathimini katika maeneo yake mapema kwani hatoweza kuvumilia mtendaji anayemkwamisha katika kuiendeleza Halmashauri.
Pia amewataka watendaji kwenda kusimamia zoezi la uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza na awali na kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kuanza shule januari anaaanza shule kipindi hicho.
Aidha, amewataka kusaidiana na walimu kuhakikisha wanamaliza suala la wanafunzi watoro kwa kushirikiana na waratibu elimu kata katika maeneo yao ili kudhibiti walimu wenye utoro wa rejareja.
" Walimu watoro ndiyo wanaotukwamisha katika suala la matokeo nataka mwakani kwa upande wa Sekondari tufike asilimia 80% ya ufaulu na 90% kwa shule za msingi sitofumbia macho uzembe wowote" amesema Chezue.
Wakati huo huo amewataka watendaji kufuata taratibu za kuomba ufadhili wa kujengewa au kuendelezewa majengo katika maeneo yao.
" Unashida ya jengo omba kwangu na si kwenda kuomba msaada nje ya Wilaya bila ofisi yangu kufahamu au Ofisi ya Mbunge hili jambo limetokea lisije kujirudia kwa namna yoyote atujashidwa mambo yetu mpaka tukaombe msaada kwenye Wilaya zingine.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa