Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe amehitimisha kambi ya UMISSETA 2024 leo June 4, 2024.
Kambi hiyo iliwekwa katika Shule ya Sekondari Ruangwa ambayo ilianza Mei 25, 2024 ikiwa na wanafunzi washiriki 216 kutoka shule mbalimbali na mpaka kufikia hatua ya kuhitimisha kambi hiyo wamebaki wanafunzi 120 pekee ambao wanaendelea kuiwakilisha Wilaya katika ngazi ya Mkoa.
Aidha, Mhe. Chikongwe ametoa zawadi ya vitafunwa kwa wanafunzi hao kutoka ABJ Kizota Bakery, "Fahari ya Nandagala" ambavyo vitawasaidia kama vifungua kinywa kabla ya kuanza safari yao mapema kesho.
Kwa upande wake, Afisa Michezo Wilaya Ndugu Shaban Mchinama ametoa wito kwa wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo kutokukata tamaa ili kujihakikishia ushindi kwani Wilaya inawategemea na ina imani watarudi na makombe ya ushindi na wataendelea na mashindano katika ngazi ya Taifa ambayo, kwa mwaka huu yatafanyika mkoani Tabora.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa kambi ya UMISSETA Wilaya Mwalimu Grayson Francis Lukoya amesema wamefanya maandalizi ya kutosha katika michezo yote wanayokwenda kushiriki na kuahidi kuchukua ubingwa kwa kishindo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa