Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Andrea Godfrey Chezue amewaaasa Walimu na kuwataka kuwa na nidhamu katika maeneo yao ya kazini na hata nje ya kazini kwani hii itasaidia kuweza kurekebisha nidhamu kwa Wanafunzi wanaowafundisha.
Alisema Mwalimu mwenye nidhamu ni rahisi kumfanya Mwanafunzi anaemfundisha kuwa na nidhamu ambayo itapelekea kuongeza kiwango cha ufaulu katika mitihani ya ndani na nje ya shule.
Hayo ameyaongea wakati wa kikao cha wadau wa elimu kilichohusisha Waratibu Elimu Kata, Wataaluma, Wakuu wa shule na Makamu kilichofanyika katika ukumbi wa Rutesco kikiwa na lengo la kuangalia njia za kuweza kutoka katika hali ya ufaulu wa sasa uliopo na kufikia nafasi nzuri zaidi.
Naye Afisa Utumishi wa Wilaya ya Ruangwa, Festo Mwangalika amewataka Walimu kutenga muda wa kuzungumza na Wanafunzi wanaowafundisha pale ambapo wanakuwa wamewakosea kwani hii inaaweza ikasaidia kubadili mienendo mimbovu ya Wanafunzi.
Pia aliwaambia Walimu na Waratibu Elimu Kata kuweza kuwafuatilia Wanafunzi wanaowafundisha ili kuweza kubaini wenye tabia mbovu na kuwasaidia mapema kwani hii itasaidia hata kuongeza ufaulu wa Wanafunzi kwani Mwanafunzi mwenye adabu ni rahisi kuwa na maendeleo mazuri.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari, Bi. Hawa Mchopa Bi Zena alisema ilikuweza kuongeza kiwango cha ufaulu katika Wilaya ya Ruangwa inatakiwa Wazazi wawape Walimu ushirikiano katika malezi ya Wanafunzi hao ili kuweza kufikia lengo
Kwani Watoto hawalelewi na Walimu na Wazazi tu , bali malezi ya Moto ni yajamii nzima, hivyo Jamii inatakiwa kutoa ushirikiano katika malezi hii itasaidia kutoka katika eneo moja kwenda eneo jingine katika hali ya ufaulu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa