Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Hashim Mgandilwa amewataka vijana kuendeleza kuku waliopewa kwa ajili ya kufuga na shirika la Aghakani kutoka katika idadi ya 10 na kufika katika idadi kubwa zaidi
Amewaasa kuacha kujibweteka na kufanya kazi kwa juhudu wakiwa na umri huo wenye nguvu na kukiendeleza walichopewa Ili waweze kufikia malengo yao.
Amesema hayo tarehe 13/06/2019 wakati akifunga mafunzo ya ujasiriamali ya ufugaji kuku yaliyofanyika Ruangwa mjini ukumbi wa CCM.
Alisema mheshimiwa Mgandilwa kuna idadi kubwa ya vijana waliolala sasa wakisubiri kuanza kujishughulisha wakiwa wazee na ndiyo maana ukienda mitaani utakuwa vijana wanazurura wazee wanaenda shamba.
Pia amewataka kuwa na utunzaji na matumizi ya fedha vizuri waunayoipata bila kuangalia kama ni ndogo au kubwa
"Tengenezeni vifaraga hivyo kama mtaji wenu hamuitaji mtaji mwingine hao hao kuku 10 mnaweza wazalisha wakafika wengi msiwakatishe tamaa watu wanaowapa msaada hiyo Aghakan inajitoa msiwaangushe"
Na yoyote atakaepata shida katika kuku awe mgonjwa au amekufa awasiliane na afisa mifugo wa wilaya kutoa taarifa ikifika mwezi wa mwezi wa saba au wanane nitaanza kupita kwa kila mshiriki kujua maendeleo ya kuku na mafanikio yake.
sambamba na hayo Mhe, Mgandilwa alishukuru shirika la Aghakan kwa msaada wanaotoa hapa Wilayani kwa wananchi kwasababu wanagusa maisha ya watu moja kwa moja na kuinua vipato vya watu Wilayani humo.
Aidha aliliomba shirika hilo kutoa pia mafunzo ya kuhusu elimu ya masoko na thamani yake wakulima ili wakulima wajue lini na muda sahihi wa kulima zao fulani.
Naye afisa miradi kilimo ni biashara kutoka shirika la Aghakani kelvin baasa amewataka vijana hao waliopata fursa ya kupata mafunzo hayo kuwa mabalozi kwa vijana wenzao katika kusambaza elimu waliyoipata.
Ndg, Kelvin alisema Aghakani iliendesha mafunzo ya siku 3 ya namna ya ufungaji kuku iliyoshirikisha wajasiriamali 60. na kila mshiriki amepata kuku 10 jumla na jumla ya kuku waliogaiwa ni 600.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa