Ndg, Nicolasco Damiani Kilumile
Wilaya ya Ruangwa ina eneo linalofaa kwa kilimo kwa mazao ya chakula na biashara lenye ukubwa wa hekta 204,486. Mazao yanayo zalishwa sana ni Korosho, ufuta, muhogo, Alizeti na mahindi na kilimo cha mbogamboga na matunda. Uwepo wa bonde la mto Mbwemkuru na Lukuledi inawezesha kufanya kilimo cha umwagiliaji.
Eneo lenye ukubwa hekta 35,559 limetengwa kwa ajili ya kilimo cha Muhogo katika kata za Narungombe, Chibula, Chienjere, Namichiga na Mbekenyera. Pia eneo lenye ukubwa wa hekta 10,872 limetengwa kwa ajili ya kilimo cha Ufuta katika kata za Nambilanje, Mbwemkuru na Chunyu. Maeneo mengine yanayofaa kwa kilimo cha Mbogamboga ni katika kata ya Nkowe, Mnacho na Likunja ambapo nyanya na vitunguu uzalishwa kwa wingi.
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA
JINSI HUDUMA ZINAVYOPATIKANA
Huduma hizi hutolewa ndani ya Wilaya kwa njia zifuatazo
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa