Ndg. Lawrence Mapunda
Mkuu wa Idara ya Maji.
SEKTA YA MAJI
1.0 HALI YA HUDUMA YA MAJI WILAYANI
Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wanapata huduma ya maji safi na salama kutoka katika vyanzo vifuatavyo; Visima vifupi, Visima vya kati, Visima virefu ambavyo vimefungwa pampu za mikono, Miradi ya maji bomba ya maporomoko (Gravity schemes) na miradi ya maji ya kusukumwa na mitambo (Pumping schemes).
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Ruangwa kwa ujumla inakadiriwa kufikia asilimia 51.43 sawa na watu 71,244 mwezi Novemba, 2018 kutoka asilimia 38.8 zilizokuwepo mwaka 2015 sawa na watu 50,859
2.0 UTOAJI WA HUDUMA YA MAJI WILAYANI UMEGAWANYIKA KATIKA MAENEO MAWILI
2.1 HUDUMA YA MAJI VIJIJINI (IDARA YA MAJI)
2.1.1 Majukumu ya Idara ya Maji
i) Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Maji.
ii) Kutayarisha bajeti ya maji ya Halmashauri ya Wilaya.
iii) Kusimamia utayarishaji na usanifu wa miradi ya maji pamoja na kusimamia ujenzi wake kwa kuzingatia maombi kutoka vijijini.
iv) Kutoa mafunzo na utaalam kwa jamii katika utekelezaji wa miradi ya maji vijijini.
v) Kusimamia ujenzi wa miradi inayotekelezwa na wakandarasi.
vi) Kusimamia kazi za Wataalam Washauri na wakandarasi walioajiriwa na Halmashauri wanaotekeleza kazi za maji.
vii) Kufuatilia shughuli za sekta binafsi mbalimbali wanaofanya shughuli za maji na kutoa ushauri.
viii) Kusaidia vijiji kuunda vyombo vya uendeshaji wa miradi ya maji
ix) Kutayarisha miongozo ya uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji itakayosaidia vijiji.
x) Kusaidia vijiji kuhusu namna ya kushirikiana na vyombo na mashirika mbalimbali
xi) Kutayarisha taarifa za kila mwezi kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya na kupeleka nakala mkoani na wizarani.
xii) Kushauri Halmashauri kuhusu ajira ya wataalam mbalimbali wa maji kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Maji.
2.1.2 Mafanikio ya Idara ya Maji kwa kipindi cha awamu ya tano
(2015 – Disemba, 2018)
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini imeongezeka kutoka 38.5% mwaka 2015 hadi kufikia 51.20% kufikia mwezi Novemba, 2018 ikiwa ni ongezeko la 12.7% ambapo jumla watu 64,498 waishio vijijini wanapata huduma ya maji.
Katika kipindi cha awamu ya tano kazi zifuatazo zimetekelezwa:-
i. Upanuzi (Extension) wa mradi wa maji kutoka Mradi wa Maji wa Mbwinji kuelekea vijiji vya Litama, Likwachu, Chiapi, Nandanga, Luchelegwa, Ipingo na Mbecha. Umekamilika mwezi Mei, 2018 na jumla ya watu 6,111 wananufaika na mradi huu. Mradi huu umetekelezwa kupitia Mamlaka ya Maji Masasi na Nachingwea (MANAWASA).
ii. Jumla ya miradi mikubwa 2 ya maji imekamilika mwaka 2016. Miradi iliyokamilika ni mradi wa maji Mandawa ambao unahudumia vijiji 5 vya Nahanga, Mchichili, Mtondo, Mandawa chini na Chikundi pamoja na mradi wa maji kijiji cha Mihewe. Jumla ya Tsh 1,747,008,626.39 zimetumika. Miradi hii inawanufaisha jumla ya watu 13,756.
iii. Ujenzi wa Mradi wa Maji Mbekenyera - Naunambe umekamilika mwezi Juni, 2018 na wananchi 7,000 wameanza kupata maji na salama.Jumla ya Tsh. 828,019,707.78 zimetumika.
iv. Ujenzi wa Miradi ya maji katika vijiji vya Chienjere, Namilema, Nangumbu na Narungombe umeanza. Miradi hii kwa pamoja inagharimu jumla ya shilingi 1,405,583,235.00 na ikikamilika itahudumia jumla ya watu 35,760.
v. Ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mibure, Namakuku na Namahema umekamilika na jumla ya watu 6,133 wananufaika.Jumla ya Tsh. 631,593,444.50 zimetumika.
vi. Ukarabati wa mradi wa maji wa Michenga ‘A’ na Michenga ‘B’ umekamilika na wananchi wapatao 3,228 wanapata huduma ya maji safi. Awamu ya kwanza ya mradi wa maji wa vijiji vya Nangumbu A, Nangumbu B na Mtakuja umekamilika. Miradi yote miwili imetekelezwa kwa fedha za msaada kutoka ubalozi wa Japan wa shilingi 173,585,406 na Tsh 28,043,814 mchango wa Halmashauri. Jumla ya Tsh. 116,475,000 zimetumika kukarabati mradi wa Michenga na Tsh. 97,472,606 zimetumika kujenga awamu ya kwanza wa mradi wa maji Nangumbu.
vii. Kazi ya Utafiti na Uchimbaji wa visima vya maji vitakavyofungwa pampu za mkono kupitia shirika la GAiN (Global Aids Network) inaendelea. Hadi mwezi Oktoba, 2018 jumla ya Visima 62 vimechimbwa. kati ya hivyo visima 42 vimekamilika na vinatumika, visima 15 vimechimbwa bado havijafungwa Pampu za mikono na Visima 5 havikuwa na maji. Orodha ya vijiji ambavyo vimechimbiwa visima imeambatanishwa.
Mheshimiwa Mbunge kwa kushirikiana na Halmashuri wamechimba visima 4 kwenye vijiji vya Nanganga, Malolo, Mbecha, na Manokwe ambavyo vimefungwa pampu za mikono. Visima vimekamilika na vinatumika. Jumla ya watu 5,180 wananufaika.
ix. Taasisi ya AFICAN MUSLIM AGENCY imechimba visima 3 kwenye vijiji vya Lipande, Namilema na kitongoji cha Matumbu na imejenga imejenga mradi 1 wa maji mdogo kwenye kijiji cha Nkowe
x. Taasisi ya REHEMA fOUNDATION imechimba visima 2 na kujenga miradi midogo kwenye Shule ya Msingi Mandarawe na Shule ya Msingi Mnacho.
xi. Vyombo 17 vya watumiaji maji vimeundwa kwenye miradi mikubwa na midogo ya maji ambayo ujenzi wake umekamilika na inatumika. Vyombo hivyo vina jumla shilingi 33,928,248.14 ambazo zipo benki kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya mairadi ya maji.
xii. Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) limechimba visima 6 na kufunga Pampu za mikono katika vijiji 6 vya Nandenje, Mandarawe, Mbekenyera, Namichiga, Mkaranga na Nanjaru.
Kampuni ya Madini ya LINDI JUMBO imechimba visima viwili na kufunga Pampu za mikono katika vijiji vya Matambarale kusini na Namkonjela.
Visima 3 vimechimbwa kwenye vijiji vya Mpumbe, Namichiga na Ruangwa Sekondari kupitia fedha za Serikali kuu. Usanifu wa mradi wa maji kwa ajili ya Shule ya Sekondari Nkowe na Ruangwa Sekondari umekamilika. Jumla ya Tsh 58,000,000 zitatumika kugharamia kazi ya uchimbaji wa visima hivyo.
2.1.3 Lengo Kuu la Idara ya Maji
Kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka 51.2% ya sasa hadi kufikia 70% ifikapo Juni, 2019 na 90.8% ifikapo Juni 2020 kama malengo ya Serikali na Ilani ya Chama Tawala (CCM) inavyotutaka.
2.2 HUDUMA YA MAJI MJINI (MAMLAKA YA MAJI RUANGWA)
Mamlaka ya maji Ruangwa ilianzishwa kwa sheria Na. 8 ya mwaka 1997, ambayo ilirekebishwa kwa sheria Na. 12 ya mwaka 2009 na kutangazwa katika tangazo la Serikali Na. 168 la tarehe 17/06/2005. Mamlaka ya Maji Ruangwa ipo daraja ‘C’ yaani itabeba gharama zote za uendeshaji na matengenezo isipokuwa mishahara ya wafanyakazi walioajiriwa na malipo ya umeme.
2.2.1 Majukumu ya Mamlaka ya Maji Ruangwa
2.2.2 Mafanikio ya Idara ya Maji kwa kipindi cha awamu ya tano
(2015 – Disemba, 2018)
Jumla ya wakazi 8,062 kati ya wakazi 14,554 waishio Ruangwa mjini wananufaika na huduma ya maji, hivyo kiwango cha upatikanaji wa maji imeongezeka kutoka 37% mwaka 2015 hadi 55.4% Desemba, 2018 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.4
Katika kipindi cha awamu ya tano kazi zilizofanyika ni;-
2.2.3 Lengo kuu la Mamlaka ya Maji Ruangwa
Kuboresha huduma ya maji katika mji wa Ruangwa kwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 55.4 ya sasa hadi kufikia asilimia 90 mwaka 2020 kama malengo ya Serikali na Ilani ya Chama Tawala (CCM) inavyotutaka.
Karibu Idara ya maji Tukuhudumie
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa