Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inawatangazia wananchi wote wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi nafasi za kazi za Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ukiwa ni Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii nchini.
Wahudumu wapatao 872 wanatarajiwa kuchaguliwa kutoka Vitongoji 436 vya Wilaya ya Ruangwa.
Hivyo basi, Wananchi wote wakiwemo watu wenye ulemavu kutoka Vitongoji vyote wilayani Ruangwa wenye sifa stahiki wanahimizwa kuomba nafasi za Wahudumu wa Afya.
Maombi yote yawasilishwe kwa Maafisa Watendaji wa Kata ambao watasimamia zoezi la kuchagua Wahudumu wenye sifa miongoni mwa waliotuma maombi kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa