Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mwalimu George Mbesigwa amewataka vijana waliopata nafasi ya kusoma VETA ya Nandagala kuhakikisha siku ya kufungua chuo tarehe 1/06/2022 kufika chuoni hapo bila kukosa.
Ameyasema hayo wakati wa Kufunga mafunzo ya ufugaji kuki na samaki yaliyofanyika chuoni hapo kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 17 mpaka 21 mwaka huu yaliyojumuisha kata 9 ambazo ni Nandagala, Malolo, Mnacho, Namahema, Chimbila, Likunja, Nkowe, Ruangwa na Nachingwea
Alisema vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo ya kufika chuo mapema maana ikitokea mtu ajafika basi nafasi yake atapewa mtu mwingine.
"Tunajua VETA inafunguliwa mwezi wa 6 vijana mliopata nafasi mjiandae mapema msijepoteza nafasi hii kwani msipokuja nafasi hii watapewa vijana wa maeneo mengine" amesema Mbesigwa.
Vilevile alisema anategemea washiriki kwa mafunzo waliyoyapata mtaenda kufanya kwa vitendo na kuwarithisha wananchi wengine ujuzi mliopata.
"Mafunzo haya yangeweza kupelekwa sehemu nyingine ila yameletwa Ruangwa hivyo ni wajibu wenu kuyafanya mafunzo haya endelevu nendeni mkafuge kuku na samaki kama mafunzo mlivyopata" amesema Mbesigwa
Aidha aliuomba uongozi wa VETA Kanda ya Kusini Mashariki kuhakikisha Kata 13 zilizobaki zinapatiwa mafunzo kama haya na mengineyo.
Naye mratibu wa Mafunzo prosper Saki amesema amevutiwa na uitikio wa washiriki Ruangwa wamekuwa wengi tofauti na sehemu nyingine ambavyo washirikia wengi wanakuwa 30 ila Ruangwa tunawashiriki zaid ya 200.
Aliendelea kusema kutokana na mwitikio huu umemfanya atamani kurudi Ruangwa na mafunzo kama haya au mengine.
Pia aliwataka washiriki kuendeleza walichokipata katika mafunzo na si kukikalia kwasababu mshiriki anaweza kufuga kuku na samaki na akaendelea kufanya shughuli nyingine za kujipatia kipato.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa