Wananchi wa Kata ya Luchelegwa waridhishwa na ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ya Kijiji kwa Kijiji ambapo leo Agosti 13, 2024 ametembelea na kufanya Mikutano katika Kijiji cha Luchelegwa, Nandanga na Ipingo.
Ziara hiyo ina lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchi katika Vijiji husika.
Miongoni mwa kero zilizobainishwa na wananchi wa Vijiji hivyo ni pamoja na ubovu wa miundombinu, ukosefu wa ubunifu wa Maafisa Ugani, uhaba wa watumishi, ukosefu wa gari la wagonjwa, upungufu wa huduma ya maji kwa wakati, uhaba wa vilula vya maji upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa na uchakavu wa Zahanati.
Katika hatua nyingine, wananchi wamejibiwa kero na changamoto zao na wakuu wa Idara husika na kuwaahidi changamoto zao kwa wakati kwa wakati.
Aidha, Mhe. Ngoma amekagua ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Luchelegwa na kukagua ujenzi wa vyoo 13 na madarasa 3 Shule ya msingi Nandanga na kumuagiza Mhandisi Noel Kitundu kufuatilia ujenzi na kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na huduma za miradi hiyo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa