Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma ameagiza watumishi wa serikali kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za kiutumishi.
Ameagiza hilo wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa kijiji cha Chinongwe, Luchelegwa na Ipingo alipofanya mikutano ya hadhara leo tarehe 14/06/2022
Mheshimiwa Ngoma alisema watumishi wa umma waache kutumia ofisi za serikali vibaya kwani wamewekwa hapo kwa ajili ya kuhudumia na kulinda masilahi ya wananchi.
"Acheni umungu mtu fanyeni kazini acheni kujitunisha na kujiona nyie ndiyo wenyewe hapo mlipo, mmewekwa na wananchi ili muwahudumie acheni kujitutumua"
Alisema ni wajibu wa mtumishi kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi, muwahudumie wananchi wenu.
"Kusoma si sababu ya kudharau wengine elimu yako isaidie kutatua na kuleta maendeleo katika maeneo mnayofanyia kazi, hamtaki kushauriwa mnajitia ujuajia usio na maana wahudumieni wananchi wenu"amesema Ngoma
Aidha aliwaasa wananchi kuhudhuria mikutano ya hadhara inayoitishwa kwasababu ni haki na wajibu wa kila mwananchi kuhudhuria mikutano katika maeneo yao.
Vilevile amewataka wananchi wa Ruangwa kuendelea kujitolea katika miradi inayopelekwa katika maeneo yao.
"Ruangwa tumebahatika kupata miradi mingi ya elimu na afya, tujitolee katika kazi hizo pale inapoitajika, miradi hiyo ni kwa ajili yetu na si wanaotuletea" amesema Ngoma
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa