Wananchi wa Kijiji cha Mpara, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, leo Mei 3, 2025, wamefanya zoezi la usafi wa mazingira katika barabara kuu inayoelekea kwenye mradi wa maji wa kijiji hicho, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupita kijijini hapo Mei 28, 2025.
Zoezi hilo limeongozwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Likunja, Ndugu Vincent Nchimbi, na limehusisha wakazi wengi wa kijiji hicho wameonesha uzalendo kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli hiyo ya kijamii.
Aidha, Wananchi wamefanya kazi kwa ari na mshikamano mkubwa, wakionesha moyo wa kujitolea na kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa heshima kubwa. Usafi huo umejikita katika maeneo ya barabara na mazingira yanayozunguka miundombinu ya mradi wa maji wa kijiji.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa